Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania imebainisha kuwa, itaendelea kutoa elimu kwa kila mwananchi popote pale alipo atafikiwa ilikunufaika katika mapambano dhidi ya rushwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mapema leo Mei 26, Kaimu Mkuu wa sehemu ya Uratibu na utoaji Habari Idara ya Elimu kwa Umma, Makao Makuu TAKUKURU, Bwana. Matai Kilumbi amesema kuwa baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya ‘LONGA NASI’, alisema kuwa, ni kutoa wigo wa kutoa elimu sahihi ya mapambano hayo ya rushwa na pia kupitia kampeni hiyo, watawafikia watu wote kupitia gari maalum la ‘LONGA NASI’ kwani kutakuwa na faida kubwa.
“Mbali na kuzindua huduma hii ya LONGA NASI, pia tumezindua huduma mpya ya 113 ambayo watu watapiga simu ama kutuma ujumbe mfupi ambao utasaidia kushugulikia matatizo ya vitendo vya rushwa” alisema Bw. Matai Kilumbi.
Aidha, aliongeza kuwa, watu wanaweza kutumia huduma hiyo kwa wakati wowote na watahudumiwa moja kwa moja.
Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI' Likiwa mitaani wakati wa huduma hiyo ya LONGA NASI kwa kutoa taarifa ya rushwa -simu ya bure ya 113.
Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI'.
Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI'.
Hivyo, kwa kuendesha kampeni ya ‘LONGA NASI’, Mkakati wa Mawasiliano wa TAKUKURU utakuwa umetekelezwa ipasavyo lakini la muhimu ni kwamba jukumu la kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha umma katika kuzuia na kupambana na rushwa litakuwa limetekelezwa.
HUDUMA MPYA YA KURAHISISHA MAWASILIANO NA TAKUKURU
Sambamba na uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI, TAKUKURU tulizindua huduma mpya itakayowasaidia wananchi kutufikia kwa urahisi kupitia namba za dharura “113” au *113# ambazo ni BURE kama ifuatavyo:
- Ilivyokuwa kabla ni kwamba mwananchi anaweza kupiga namba “113” kupitia simu yake ya kiganjani au mezani na kuongea na Afisa wa TAKUKURU moja kwa moja kumweleza shida yake au kuripoti tukio la rushwa. Utaratibu au huduma hii ni kupitia mitandao ya TTCL, AIRTEL, TIGO, HALOTEL, VODACOM na ZANTEL;
- Sasa mwananchi anaweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi yaani “sms” kwenda nambari “113” ili kutoa maoni yake, kuuliza swali au kutoa taarifa.
- Na pia mwananchi kupitia simu yake ya kiganjani anaweza kutoa taarifa ya rushwa kwa kupiga *113# (USSD) na kufuata maelekezo yatakayofuatia;
OFISI MAALUM YA MAWASILIANO YA DHARURA (PCCB CALL CENTRE)
- Kutokana na kuanzishwa kwa huduma hizo tajwa, tunaamini kutakuwa na mwitikio mkubwa kwa wananchi kuwasiliana nasi. Hivyo ili kuhakikisha kuwa TAKUKURU tunatoa kutoa huduma hii kwa haraka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameanzisha ofisi maalum ya MAWASILIANO YA DHARURA (PCCB CALL CENTRE) iliyopo Makao Makuu ambayo itafanya kazi masaa ishirini na manne (24).
- Lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa za wananchi tunazopewa zinashughulikiwa haraka ikiwa ni pamoja na kuanzisha Uchunguzi.
- Natumia fursa hii kuwahimiza wananchi kuLONGA NASI bila woga lakini si kwa lengo la kumwonea mtu. Tupatieni taarifa sahihi nasi tutakulinda na tutawashughulikia wanaohusika na tuhuma hizo kwa weleni na haki.
Katika huduma ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia mfumo wa USSD - *113# - Mtoa taarifa ana haki ya kutaka atambuliwe au asitambuliwe na TAKUKURU. Iwapo mwananchi hatapenda kutambulika na TAKUKURU basi ahakikishe kuwa taarifa aliyoiwasilisha itakuwa imejitosheleza kwa kiwango Fulani vinginevyo itatuwia vigumu kupata ushirikiano wa mtoa taarifa katika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma husika.
Kaimu Mkuu wa sehemu ya Uratibu na utoaji Habari Idara ya Elimu kwa Umma, Makao Makuu TAKUKURU, Bwana. Matai Kilumbi akielezea namna walivyojipanga kusambaza elimu dhidi ya mapambano ya rushwa hapa nchini kupitia Huduma za 113 na LONGA NASI. kushoto kwake ni Afisa mahusiano wa TAKUKU, Bi. Angela Mulanduzi. Wakati wa mkutano huo leo Mei 26.2016, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment