BREAKING

Wednesday, 31 January 2024

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA MATAIFA 8 KUSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA 2024



Kuelekea Tamasha la Pasaka mwaka 2024 Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion waandaaji wa Tamasha hilo amethibitisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa  zaidi ya 8 watakuwepo kwenye Tamasha la Pasaka la mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Alex Msama kuwa maandalizi makubwa kuelekea Tamasha hilo yamekwisha fanyika kwa asilimia kubwa na watu wakae mkao wa kula kwani Tamasha la mwaka huu litakuwa na zuri na lenye shangwe kubwa sana kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.

Tamasha la mwaka huu litafanyika siku ya Jumapili ya Pasaka, huku kauli mbiu ikiwa ni ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS SAMIA S HASSAN MCHAPA KAZI



No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube