MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Hassan Jarifu, wakiwa na viongozi, wanachama wa CCM na wananchi wakienda katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewasili wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikakazi ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Chama wa wilaya hiyo.
Kinana amewasili wilayani humo leo Januari 1, 2024 akiambatana na viongozi mbalimbali wa Chama wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Akiwa wilayani humo kesho atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa ambao pia utahudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa.
No comments:
Post a Comment