BREAKING

Monday, 1 January 2024

KINANA ASHAURI WANANCHI WAPEWE NAFASI KUAMUA YANAYOHUSU MAENDELEO YAO.










MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulurhman Kinana amesema ipo haja ya kutoa fursa zaidi kwa wananchi kujiamulia mambo yanayohusu maendeleo yao.

Amesema huenda haifanyiki sawa kutowapa wananchi fursa kubwa ya kuamua mambo yanayohusu maendeleo yao, jambo ambalo linasababisha kutofikia ufumbuzi wa baadhi ya changamoto katika vitongoni, vijiji au mitaa.

Kinana ametoa ushauri huo leo Januari 1, 2024 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM na wanachi wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi baada ya kuzindua Shina la CCM Majengo Sokoni.

Kinana amesema wananchi ndio wanaojua changamoto na mahitaji yao katika ngazi ya kijiji, mtaa au kitongoji, hivyo ni vyema wakahusika moja kwa moja katika kujipangia maendeleo.

"Kiongozi unaweza ukaenda mahali na fikra zako mwenyewe ukifikiri shida ya watu ni shule, ni maji kumbe shida yao ni jambo jingine kabisa, hivyo ni lazima tuwashirikishe wananchi katika mambo yanayohusu maendeleo yao," amesisitiza.

Kauli ya Kinana imetokana na ombi la Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye aliyekiomba Chama kutazama uwezekano wa kuruhusu kutanua vijiji na vitongoni hususan katika maeneo ambayo kiutawala yamezidiwa kutokana na ukubwa wa eneo na wingi wa wananchi, hivyo yaruhusiwe kugawanywa.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube