Kampeni ya Magifti Dabodabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, imewakabidhi mamilioni yao washindi wa kampeni hiyo waliopatikana wikiendi iliyopita.
Katika tukio hilo washindi watatu, Flazia Issa, Stephano Mgova, Shabani Juma walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja na Kiungi Juma alikabidhiwa shilingi milioni tano alizojishindia.
Akiwakabidhi mfano wa hundi ya fedha walizojishindia Semaji la Kampeni hiyo, Haji Manara aliwapongeza washindi hao na kuwataka wakawe mabalozi wazuri wa kampeni kwani wao ndiyo mashuhuda wakubwa wa ukweli na uwazi wa kampeni hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa za Tigo, Ndevorael Eliakimu aliwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo kwa huduma mbalimbali kama vile kufanya miamala, kulipa bili na malipo mengine, kununua vocha kwa kutumia Tigo Pesa au za kukwangua na huduma nyinginezo.
Eliakimu amesema kampeni bado inaendelea ambapo pamoja na pesa taslimu kuna zawadi za seti ya vifaa vya nyumbani vya kisasa kutoka Kampuni ya Hisense ikiwemo friji, runinga, microwave na seti ya muziki (sound bar).
Sambamba na zawadi hizo, Eliakimu amesema kuna zawadi kubwa za magari mapya kabisa ya kisasa ambapo zawadi zote hizo zitatolewa mara mbili kwa kila mshindi na mpendwa wake kama inavyoitwa kampeni hiyo Magifti Dabo dabo.
No comments:
Post a Comment