BREAKING
ROSE MHANDO :MSAMA NI BABA KWANGU ACHENI KUNIGOMBISHA NAYE.   UPANDIKIZAJI WA MENO BANDIA KWA NJIA YA KISASA MUHIMBILI MLOGANZILA 45 KUNUFAIKA NA HUDUMA    UTEKAJI WA WATOTO MKUU WA MKOA WA MBEYA JUMA HOMERA AWATAKA WANAFUNZI WA HOLY LAND PRE- & PRIMARY SCHOOL KUKATAA LIFTI   MSAMA ANG'AKA WAIMBAJI WA IN JILI KUPOTOKA MAADILI   DCEA YAFANIKIWA OPERESHENI DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA JAHAZI DAWA ZA KULEVYA   NAIBU WAZIRI MKUU AKARIPIA UZEMBE TANESCO   MHE. RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZA NA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING    MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI CHINA..   RAIS SAMIA NCHINI KENYA-ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI   RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA-KENYA    Blogger Tips and Tricks & Blogger Templates

Monday, April 07, 2025

Saturday, 6 January 2024

DKT. BITEKO- TUYAENZI NA KUYALINDA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuyaenzi, kuyalinda na kuyaishi kwa dhamira ya dhati, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwani Waasisi wa Nchi  walifanya mapinduzi hayo ili kuwa na Taifa huru ambalo kila mtu anakuwa na hadhi, kuondoa dhuluma iliyokuwepo na kufanya wananchi kuishi kwa amani na furaha.

Amesema hayo tarehe 6 Januari 2024 wakati akizungumza na Wananchi  katika Wilaya ya Mkoani, mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua Afisi ya Uhamiaji na Makaazi ya Askari wilayani humo.

“Sisi Wananchi tunawajibu wa kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuyaishi, kuyaheshimu,  kukuza uchumi wa nchi na kukuza uzalendo ili baada ya muda mrefu hata baada ya miaka 100 mbele, watakaokuja kusherehekea Mapinduzi haya wakute Zanzibar iliyobora zaidi na waseme Mapinduzi haya yalitufaa.” Amesema Dkt. Biteko

Ameeleza kuwa, moja ya tunu tuliyonayo ni mshikamano hivyo watu wasiruhusu mtu yoyote kuwagawanya kwa misingi yoyote ile, bali maendeleo yaunganishe watu wote na kwamba tofauti za vyama, dini na  kabila visifanye watu wakae kwenye makundi bali kuunganisha watu kwa maslahi ya nchi na watanzania.

Amesema kuwa, nchi inapoenda kusherehekea Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari mwaka huu, watanzania wote waungane kuwaombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, ili waendelee kuongoza vyema, kuimarisha ustawi wa Taifa na kuwaunganisha Watanzania.

Kuhusu Jengo hilo jipya la Afisi ya Uhamiaji katika Wilaya ya Mkoani, mkoani Kusini Pemba, Dkt, Biteko amesema kuwa ni moja ya matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani kabla ya Mapinduzi watu walinyimwa haki zao za kimsingi zikiwemo za uhamiaji kama vile kupata pasi ya kusafiria na hivyo Mapinduzi yamewezesha wananchi kupata uhuru wa kusafiri nje ya mipaka ya nchi.


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube