Klabu ya Rotary Tanzania imekabidhi msaada wa wa Madawati mia moja katika shule ya msingi mtakuja iliyopo Kata ya kunduchi Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wao wa kurudisha kwa Jamiii
Akingumza kwa niaba ya Klabu hiyo Ezra Kavana ambaye ni Mkurugenzi wa vijana Rotary amesema mbali na kutoa msaada wa madawati hayo wametoa vitabu mia tano vya hadithi ,mipira kumi na kalamu elfu moja
Ameongezea kwa kusema msaada huo unalenga kuonyesha mchango wao katika jamii na kuisaidia huku Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Anna Hendry akibainisha kwamba Msaada huo utawasaidia katika elimu akitumia wasaa huo kuwaomba wanajamii na taasisi zingine kuwa unga mkono.
No comments:
Post a Comment