Miezi kadhaa iliyopita King wa Bongo Flava Ali Kiba alitangaza rasmi ujio wa ngoma yake na mwanamuziki mkongwe, maarufu na wa zamani kutoka Afrika ya Kusini Yvonne Chakachaka. Hii ilikuwa ni hatua muhimu sana ya kimuziki kwa nguli huyo wa muziki kutoka Tanzania katika juhudi za kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya mipaka, lakini pia kuuthibitisha umma juu ya uwezo wake kimuziki.
Lakini inaonekana kwamba Yvonne Chakachaka aliyetamba na nyimbo kama "Mama Afrika", "Thank you Mr. Dj" na "Umqombothi" miaka ya 80, amevutiwa sana na muziki wa Bongo na hivyo kuwa tayari kufanya kazi na wasanii wengine kutoka hapa nchini. Hii inathibitika baada ya hivi karibuni, kupitia account yake ya instagram kuonesha kuwa yuko studio na moja ya wasanii wa Tanzania, Otuck William, wakirekodi wimbo. Legend huyo wa muziki wa Africa AKA "The Princess of Africa" aliandika, "Spending some time with my son @otuck_william in Kigali, doing some work for the youth. Day well spent, thank you @mrmingz".
Yvonne Chakachaka alikua jijini Kigali, nchini Rwanda kwa ajili ya onesho na kukutana na Otuck, ambaye pia alikua huko kwenye shughuli zake za kikazi na kimuziki, hivyo tutegemee kikubwa kutoka kwa hivi vichwa viwili. Otuck ni msanii mkongwe wa RnB nchini anayetambulika sana na ngoma zake kama Deja Vu, Roho Juu alitomshirikisha Heri Muziki na So Cold aliyoitoa hivi karibuni. |
No comments:
Post a Comment