Mchambuzi na mwandishi wa ripoti ya utafiti wa Uhisania Tanzania Bw. Tom Were akiichambua ripoti hiyo mapema jana jiji Dar es salaam.
Watanzania
wametakiwa kuwa na moyo wa kutoa kwa kusaidiana wenyewe ndani ya jamii na hata
katika kuendeleza huduma mbalimbali za kijamii ili kuweza kusaidia taifa
kusonga mbele.
Hayo
yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Mwanachama wa Bodi ya wakurugenzi ya Foundation
for Civil Society Bi. Nesia Mahenge wakati wa uzinduzi wa riporti ya utafiti
maalum kuhusu uhisani na utamaduni wa kujitolea ndani ya Tanzania.
Ripoti hiyo
iliyohusisha utafiti uliofanywa kati ya mwezi februari hadi mwezi aprili na kuhusisha
mashirika ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Jukwaa la Uhisani
Tanzania (Tanzania Philanthropy Forum) kwa lengo la kupata taarifa muhimu
kuhusu hali ya uhisani au hali ya kujitolea kwa jamii nchini Tanzania.
Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Nesia Mahenge akielezea kwa undani mambo yanayopatikana katika ripoti hiyo ya Utafiti wa Uhisani nchini Tanzania.
Mwanachama
wa bodi huyo alisisitiza umuhimu wa mtu mmoja mmoja pamoja na taasisi mbalimbali binafsi hususani
zinazofanya kazi za kijamii kuendelea kujitolea katika miradi mbalimbali ya
maendeleo na kuacha tabia ya kuisubiri serikali kufanya kila kitu.
Aliendelea
kusisitiza kuwa ni vema kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta
maendeleo ikiwa ni moja wapo ya njia nzuri ya kuisaidia serikali katika kuinua
miradi kadhaa ikiwemo Elimu, Afya, Ujenzi na sio kwa kuwezesha kifedha tu
lakini hata katika kusaidia kuleta wahisani watakao fanikisha zoezi hilo pia ni
hatua kubwa.
“Lakini pia
katika hali ya kujitolea kwa Tanzania uelekeo wake sio mbaya sana kwani
watanzania wanaonyesha kuwa wana moyo wa kutoa kwa kusaidiana, lakini pia hata
katika juhudi za kujiletea maendeleo kwa kusaidia huduma mbalimbali za kijamii
hali inaonyesha bado tupo vizuri” alisema Nesia
Wachambuzi wakiichambua Ripoti ya Utafiti wa Uhisani Tanzania
Aliongezea
kwamba tatizo moja linalojitokeza katika nchi yetu ni kwamba kunakosekana
takwimu/taarifa sahihi za watu wanaojitolea lakini zingekuwepo ingesaidia kujua
kiwango husika cha watu wanaojitolea katika miradi ndani ya jamii yao na hii
inatokana na sharia na mifumo iliyowekwa ndani ya nchi yetu.
Na mwisho
alipenda kuwashauri wadau kutumia matokeo ya utafiti huu kama sehemu ya
kubadilishana uzoefu katika tasnia nzima ya uhisani na kujitolea katika jamii
na kuhamasisha umuhimu wa uhisani miongoni mwa jamii ya watoaji pia kuweka
muongozo wa kuendeleza uhisani Tanzania.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini uchambuzi wa Ripoti ya uhisani Tanzania iliyozindiliwa na Foundation for Civil Society mapama jana jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment