BREAKING

Thursday 28 June 2018

MULTICHOICE TANZANIA YAWEKA NGUVU KWENYE RIADHA


Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wapili kushoto) na Kocha wa riadha Meta Petro (kulia) ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano wakisaini mkataba maalum wa udhamini wa mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha. Kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida Buday na wa pili kushoto ni mwanariadha Fracis Damas Damiano.

 

 Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wapili kushoto) na Kocha wa riadha Meta Petro (kulia) ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano wakiwa Tayari kubadilishana nyaraka punde baada ya kusaini  mkataba maalum wa udhamini wa mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha. Kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida Buday.


Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (kushoto) akimkabidhi nakala ya mkataba mwanariadha chipukizi Francis Damiano mara tu baada ya kusainia mkataba wa udhamini kwa mwanariadha huyo. Kulia ni Kocha wa riadha Meta Petro  ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano.  Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha.

MultiChoice Tanzania imetangaza kuendelea kudhamini mchezo wa riadha hapa nchini huku ikisaini makubaliano maalum ya kumdhamini mwanariadha kinda Francis Damiano Damasi. Udhamini huo unahusisha fedha ya kujikimu kwa mawanariadha huyo na mafunzo yake na wanariadha wengine katika kambi maalum ya mafunzo inayotarajiwa kuwa wilayani Mbulu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini kwa mwanariadha huyo, Mkuu wa Mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana, amesema kuwa dhamira kubwa ya MultiChoice ni kuhakikisha kuwa mchezo wa riadha unakuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa, kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
“Tunataka taifa hili lijulikane ulimwengu mzima kama chimbuko la mabingwa, na tumeanza na riadha. Tumedhamiria kukuza mchezo huu na kuufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo, ni burudani, na ni sekta nyeti kiuchumi kama ikiendelezwa” alisema Mshana na kuongeza “Tunataka kuusikia wimbo wetu wa taifa katika mashindano makubwa ya kimataifa, tunataka kuiona bendera yetu ikipepea juu katika kila mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa, tunataka mamia ya vijana wetu wenye uwezo mkubwa katika riadha washiriki kwenye mashindano makubwa, waweze kujipatia kipato, kuwekeza na kuwa chanzo cha maelfu ya ajira na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu”
Amefafanua kuwa udhamini huo utakuwa wa mwaka mmoja na utaendelezwa na kuboreshwa kulingana na hali itakavyokuwa pamoja na mafanikio yatakayopatiokana. “ Huu ni mkakati wetu endelevu, ni mpango wetu maalum unaojulikana kama ‘Ni Zamu Yetu’! ambao umejikita katika kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika riadha.” Amesema Mshana.
Mbali na kumdhamini Damiano, MultiChoice pia itadhamini kambi maalum ya mafunzo itakayokuwa wilayani Mbulu ambayo inatarajiwa kuanza mafunzo rasmi hivi karibuni. Amebainisha kuwa taratibu za kuanza kwa kambi hiyo zipo katika hatua nzuri na kambi inatarajiwa kuanza rasmi Agosti mwaka huu na itakuwa na wanariadha kinda wasiopungua sita – wasichana na wavulana.
Kwa upande wake mwanariadha Damiano ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas, amesema udhamini huo utamfanya aweze kufanya mazoezi yake vizuri kwani sasa hyo ndiyo itakuwa kazi yake ya kudumu. Amesema kilicho mbele yake ni ushindi tu. “Nashukuru sana kwa udhamini wa MultiChoice, na mimi naahidi kuwa nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa siwaangushi MultiChoice na siwaangushi watanzania.”
Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida-Buday, amesema wamefarijika sana kuona kuwa MUltiChoice inaendelea kudhamini riadha na akasema udhamini huo siyo tu utamsaidia mwanariadha husika, bali pia ni chachu hata kwa wanariadha chipukizi kuwa na moyo na ari ya kushiriki katika mchezo huo.
Amesema Shirikisho la Riadha Tanzania litahakikisha kuwa udhamini huo unakuwa wa manufaa na unazaa matunda yaliyotarajiwa ya kuleta medali zaidi kutaka katika mashindano ya kimataifa. “Ufadhili wa aina hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa riadha. Tunaahidi ushirikiano wetu wa hali na mali ili kufanikisha malengo na tutahakikisha kuwa tunatoa ushirikiano unaostahili kwa wadhamini wetu” alisema Gida.
Mwanariadha Francis Damiano Damasi, anatarajiwa kushiriki mashindano makubwa ikiwemo Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki yanayofanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam, Mashindano ya vijana ya Dunia (World Junior Championship) mwezi Julai nchini Finland, Mashindao ya vijana ya Olympic kanda ya Afrika mwezi Julai nchini Algeria, Mashindano ya vijan ya Olympic (Youth Olympic Games) mwezi Oktoba nchini Argentina, na mashindano ya nyika ya vijana (World Junior Cross-country) mapema mwakani nchini Denmark.


NEYMAR ANG'ARA BRAZIL IKISHINDA 2-0 NA KUSONGA MBELE KOMBE LA DUNIA


Nyota wa Brazil, Neymar akimtoka kiufundi mchezaji wa Serbia katika mchezo wa Kundi E Kombe la Dunia Jumatano Uwanja wa Otkrytiye Arena mjini Moskow. Brazil ilishinda 2-0, mabao ya Paulinho dakika ya 36 na Thiago Silva dakika ya 68, hivyo kufuzu hatua ya 16 Bora na itakutana na Mexico Julai 2, wakati Serbia imetolewa. Uswisi iliyotoa sare ya 2-2 na Costa Rica nayo imefuzu pia 16 Bora na itamenyana na Sweden Julai 3 

UJERUMANI WATEMESHWA KOMBE LA DUNIA, WAPIGWA 2-0 NA KOREA KUSINI


UJERUMANI imevuliwa ubingwa wa dunia baada ya kufungwa mabao 2-0 na Korea Kusini leo katika mchezo wa Kundi F Kombe la Dunia Uwanja wa Kazan Arena nchini Urusi.
Mabao yaliyoizamisha Ujerumani waliobeba taji hilo mwaka 2014 nchini Brazil kwa kuifunga Argentina 1-0 katika fainali yamefungwa na Kim Young-Gwon dakika ya 90 (ongeza mbili za majeruhi) na Son Heung-Min dakika ya 90 ( (ongeza sita za majeruhi).
Ujerumani inatolewa mashindanoni baada ya kuambulia pointi tatu tu kutokana na ushindi wa 2-1 dhidi ya Saudi Arabia na kupoteza mechi mbili, kwani kabla ya leo walifungwa 1-0 na Mexico inayoungana na Sweden kwenda hatua ya 16 Bora.
Korea Kusini pamoja na ushindi wa leo imeaga pia mashindano, kwani imemaliza na pointi tatu sawa na Ujerumani ya kocha Joachim Low .
Hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka 80 kwa Ujeruman kutolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia. Nayo Sweden imeichapa 3-0 Mexico, mabao ya Ludwig Augustinsson dakika ya  50, Andreas Granqvist kwa penalti dakika ya 62 na Edson Álvarez aliyejifunga dakika ya 74.  

Timo Werner wa Ujerumani akisikitika baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kuwafunga Korea Kusini 

Wednesday 27 June 2018

GERMANY OUT!......NI KOMBE LA DUNIA LA MAAJABU



KWA HABARI ZAIDI INGIA HAPA>>>>>>>>>>

MULTICHOICE TANZANIA YASAIDIA KUIMARISHA ELIMU ZANZIBAR


Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetoa msaada wa jumla ya shilingi milioni 120 kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba za waalimu katika shulya Sekondari Kizimkazi iliyopo Kusini Unguja. Msaada huo utawezesha kukamilishwa kwa nyumba mbili za waalimu katika shule hiyo ambapo ujenzi wake ulikwama kutokana na ukosefu wa fedha.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuingia mkataba wa ufadhili huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kusini Diwani Juma Mussa amesema ujenzi wa nyumba utasaidia kupunguza tatizo la nyumba za walimu katika shule hiyo ambapo baadhi ya walimu hulazimika kukaa mbali na shule kutokana na ukosefu wa nyumba za walimu shuleni hapo. Amesema msaada huo unaotolewa na MultiChoice utawezesha mradi huo kukamilika kabisa ikiwemo kuwekwa kwa huduma muhimu kama umeme na maji.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Juma Musa akizumgumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania na kushoto ni Mkurugenziwa Halmashauri ya wilaya ya Kusini Kassim Mtoro. Hafla hiyo ilifanyika halmashauri ya wilaya Kusini Unguja.
Amesema ufadhili wa MultiChoice umekuja kwa wakati muafaka kwani kwani halmashauri yake ipo katika mkakati wa kuimarisha sekta za kijamii ikiwemo elimu. “Tumefurahishwa sana na ufadhili huu wa MultiChoice na tunatoa shukrani za pekee kwa kampuni hii kwa kukubali kushirikiana nasi katika kuimarisha sekta ya elimu” alisema Juma na kuongeza kuwa halmashauri yake itahakikisha fedha hizo zinatumika kwa jinsi zilivyopangiwa ili kuhakikisha kuwa wafadhili wote wanakuwa na Imani na pia waweze kuendelea kusaidia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana amesema kampuni ya MultiChoice  imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika sekta mbalimbali za kijamii, na ufadhili huu ni ishara tosha ya ushirika wao katika kuleta maendeleo ya jamii yetu.

Kutoka kulia; Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Mussa Juma na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kassom Mtoro wakiangalia waraka wa makubaliano ya ujenzi wa nyumba hizo
“Mbali na kutoa huduma zenye ubora wa kisasa za televisheni kupitia DStv,  MultiChoice pia tumewekeza katika miradi ya kijamii na tumekuwa tukifanya hivi kwa mujibu wa sera yetu inayotutaka kuhakikisha kuwa uwepo wa kampuni yetu hapa nchini unachangia katika kuleta maendeleo endelevu” alibainisha Mshana.
Mshana amesema kuwa MultiChoice inashiriki katika miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kukuza na kuimarisha vipaji katika tasnia ya michezo na filamu, miradi ya elimu, afya, mazingira pamoja na kuwawezesha vijana wa tanzania kujiajiri.
Akifafanua zaidi kuhusu Mradi huo, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kusini Kassim Mtoro amesema taratibu zote zimeshakamilika na tayari mkandarasi ameshapatikana na kazi imeanza. Amefafanua kuwa nyumba hizo  zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi familia mbili 
na hivi sasa zipo katika hatua ya kupaua.


Jengo la nyumba mbili za waalimu likiwa linaendelea kujengwa katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja kwa ufadhili wa kampuni ya MultiChoice.
Kwa mujibu wa Kassim, nyumba hizo zinatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili ijayo na wanatarajia kuwa kila kitu kitakwenda sawa kwani tayari taratibu zote zimeshakamilika kuwawezesha MutiChoice kutoa fedha hizo.

Saturday 23 June 2018

USWIZI INA JAMBO LAKE,YATOA KICHAPO SERBIA DAKIKA ZA LALA KWA BURIANI XHAKA AVUNJA REKODI YA 1996


Switzerland imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Serbia katika mchezo wa kundi E

Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Mitrovic mnamo dakika ya 5 tu ya mchezo kwa upande wa Serbia huku la Switzerland likiwekwa kimiani na Granit Xhaka mnamo dakika ya 52 kabla ya Xherdan Shaqiri kuongeza msumari wa mwisho dakika ya 90 ya mchezo

Xhaka ambaye hivi karibuni amesaini mkataba wa muda mrefu kuitumikia Arsenal ameweka rekodi ya kupiga jumla ya pasi 71 ambazo hazijapigwa na mchezaji yoyote wa Urusi katika michuano hiyo tangu 1996.

Matokeo hayo yanaifanya Uswizi kuwa pointi sawa na Brazil katika kundi E lakini ikishika namba 2 kutokana na idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

MZEE MAJUTO AWASILI AKITOKEA KWENYE MATIBABU INDIA....


Muigizaji nguli nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto amewasili nchini na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

Mzee Majuto amewasili Airport leo Juni 22, 2018 majira saa 10 jioni na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo atakua hapo kwa muda ili kukutana na wataalam kwa ajili ya uangalizi kukamilisha matibabu yake.



'NIGERIA ILITUANGUSHA MWANZO SASA NI MOTO' RAIS WA NIGERIA ALIFUNGUKA HIVYO


Dakika 90 za mchezo wa kundi D umemalizika kwa Nigeria kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Iceland.

Mechi hiyo imekuwa ya pili kwa timu kutoka Afrika kupata ushindi baada ya Senegal kuitwanga Poland 2-1 katika mchezo wa kundi H.

Mabao yote ya Nigeria yamewekwa kimiani na Ahmed Mussa katika dakika za 49 na 75.

Matokeo hayo sasa yanakuwa yanaipa unafuu Argentina ambapo kibarua chao kijacho itakuwa dhidi ya Nigeria.


Argentina imekalia mkia kwenye kundi D kutokana na kipigo cha jana dhidi ya Croatia cha mabao 3-0.

WANAMUZIKI NCHINI KUTEMBELEA BUNGE WIKI IJAYO KUPITIA TAMUFO


Rais  wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tamufo, Morocco Dar es Salaam jana wakati wa  kujadili masuala mbalimbali ya umoja huo pamoja na safari ya baadhi ya wanachama wa Tamufo kwenda Bungeni Dodoma.
Mhandisi Abdallah Ally kutoka  Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Rais  wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akiteta jambo na Katibu wa umoja huo, Stellah Joel wakati wa mkutano huo.
Msemaji wa Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii, Ahmed Kipozi  akizungumza kwenye mkutano huo
Mwanamuziki Hamza Kalala akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki.
Katibu wa umoja Tamufo, Stellah Joel, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mwanamuzi mahiri Kitenzogu Makassy, akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki Hamza Kalala.
Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Witness Kibonge, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel, akizungumza kwenye mkutano wa kujadili safari hiyo ya Bungeni Dodoma.
Wanamuziki Hamza Kalala na Mzee Makassy wakiteta jambo kwenye mkutano huo.

WANAMUZI walio wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) wiki ijayo watatembelea Bunge kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Umoja huo, Dk.Donald Kisanga alisema kwa umoja huo kwao ni fursa kubwa ya kutembelea Bunge.

"Kwetu sisi Tamufo kutembelea Bunge ni fursa kubwa na tunaenda kuona jinsi Bunge linavyofanya kazi yake" alisema Kisanga.

Kisanga alisema msafara wao utaondoka jijini Dar es Salaam Juni 23 na Bungeni watakuwepo Juni 25 mwaka huu na mwenyeji wao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe.

Kisanga aliyataja baadhi ya makundi ya wanamuziki watakaokuwepo kwenye msafara huo kuwa ni wanamuziki wa dansi ambalo litaongozwa na Mwanamuziki mkongwe Boniface 
Kikumbi Mwanza Mpango au King Kik na Hamza Kalala.

Alitaja kundi la muziki wa Injili kuwa litaongozwa na Stella Joel na Emanuel Mbasha wakati Bongo Fleva litaongozwa na Witness Kibonge Mwepesi huko taarabu likiongozwa na Sizer Masogelo na Muziki wa Asili likiongozwa na  Grace Kayinga.

Katibu wa Tamufo, Stellah Joel alisema wanamuziki kutoka mikoa yote waliotayari watakuwepo kwenye msafara huo.

DKT TIZEBA ATOA SIKU 4 WAKULIMA WA MKONGE MKOANI TANGA KULIPWA FEDHA ZAO


Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akitoa maelekezo ya serikali wakati wa kikao cha pamoja na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) kabla ya mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018. (Picha 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akizungumza jambo kabla ya kumaribisha mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kuongoza mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
Viongozi mbalimbali Mkoani Tanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakiagana na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
Wadau wa zao la Mkonge wakichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.

Wakulima wa Mkonge Mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kupitia agizo lake alilolitoa kwa Kampuni ya Katani Limited kuhusu kulipa madeni ya wakulima ndani ya siku nne kuanzia 21 Juni 2018 hadi 26 Juni 2018 Kwa madeni ya muda mrefu ya wakulima wa zao hilo jambo lililopelekea kupunguza ufanisi na tija ya Kilimo Kwa wakulima hao.

Dkt Tizeba ametoa agizo hilo leo 21 Juni 2018 akiwa kwenye mkutano na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) unaotekelezwa kwenye mashamba matano ya Hale, Magunga, Magoma, Mwelya na Ngombezi yaliyo chini ya miliki ya Bodi ya Mkonge Tanzania. 

Katika Mkutano huu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Martin Shigela sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe, Msajili wa Hazina, Mtendaji wa BRELA, Muwakilishi wa mwanasheria Mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge na wataalamu wengine; Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba ametoa agizo hilo Kwa Uongozi wa mfumo wa Kilimo cha wakulima wadogo wa kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO), Kampuni ya Katani ltd ambayo ndio mnunuzi pekee wa Mkonge wa mkulima na Bodi ya Mkonge Tanzania.

Sambamba na agizo hilo pia Mhe Waziri ameiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania kupitia upya mikataba yote iliyopo Kwa kushirikisha Bodi yenyewe, Kampuni ya Katani na wadau wa zao hilo haraka iwezekanavyo ili kurekebisha makosa yaliyopo.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo ya Mkonge Tanzania kuitisha kikao na wadau wote wa zao hilo ili kupitia upya utaratibu wa makato ya mgawanyo wa mapato katika kusindika zao la Mkonge.

Mhe Dkt Tizeba aliongeza kuwa hati za miliki ya mashamba zitapaswa kutolewa Kwa wahusika Mara baada ya kujiridhisha na mchakato utakapokamilika huku akiwataka wakulima kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Tanga huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela Kwa umakini na uwajibikaji katika kusimamia sekta ya Kilimo hususani zao la Mkonge mkoani humo.


Wednesday 13 June 2018

MOHAMED SALAH VIPIMO VYA BEGA LAKE VINARIDHISHA ......

Mohamed Salah has his left shoulder checked out by an Egypt team physio on Tuesday
Mohamed Salah aendelea kufanyiwa vipimo via bega lake, kuelekea mechi za Kombe la Dunia KWA MIPCHA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>> 

JULEN LOPETEGUI KOCHA MPYA WA MADRID




 Kocha Julen Lopetegui ametangazwa kuchukua mikoba ya Kocha Zinedine Zidane aliyeamua kuachia ngazi.

Lopetegui mwenye umri wa miaka 51 kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Hispania inayoshiriki Kombe la Dunia.

Kocha huyo kijana ataanza kazi mara moja baada ya michuano ya Kombe la Dunia.

Baada ya kujiuzulu kwa Zidane Mei 31, mwaka huu kulikuwa na majina ya makocha wengi kama Antonio Conte wa Chelsea, Jurgen Klopp wa Liverpool na Mauricio Pochettino wa Tottenham alipewa nafasi kubwa.

DKT TIZEBA AFUNGUA MASOKO YA TUMBAKU KITAIFA WILAYANI KAHAMA



Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akimkabidhi cheti cha pongezi Mkulima Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ambaye ameshika nafasi ya tatu katika msimu wa kilimo cha tumbaku wa mwaka 2017/2018 wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikata utepew kuashiria ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa katika sherehe iliyofanyika kwenye viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akishuhudia ununuzi wa tumbaku wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Baadhi ya wakulima wa tumbaku wakishuhudia sherehe za uzinduzi wa ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.

Na Mathias Canal, WK, Kahama-Shinyanga

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amefungua masoko ya tumbaku Kitaifa huku akitoa onyo kali kwa wakulima waliolima zao hilo nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu wa sheria ya zao hilo kwa kuwataka kuacha mara moja kwani serikali itashughulika na wote wanaokiuka taratibu za kilimo hicho.

Dkt Tizeba ameyasema hayo leo 12 Juni 2018 katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati akihutubia mamia ya wakulima wa tumbaku kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa.

Dkt Tizeba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack kufanya kikao na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa huo kuhakikisha wanazuia wananchi kulima nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu ya sheria ya zao la tumbaku.

Alisema kuwa wigo wa soko la tumbaku unazidi kuwa finyu kutokana na viongozi mbalimbali kuwakumbatia baadhi ya wakulima wa tumbaku wanaolima nje ya mfumo wa zao hilo.

Katika sherehe hiyo Mhe Dkt. Tizeba amekabidhi vyeti vya pongezi kwa wakulima waliofanya vizuri katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 ambao ni mkulima Emmanuel Cherehani kutoka Wilaya ya Ushetu aliyeshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ni Jimson Mwanjwenga kutoka Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wakulima wa zao la tumbaku Tanzania Kaimu Meneja Mkuu TCJE Ndg Bakari Kisia alisema kuwa zao la tumbaku limeanza kulimwa nchini Tanzania enzi za ukoloni kwa kuanzia mikoa ya Ruvuma (Tumbaku ya Moshi) na Iringa (Tumbaku ya mvuke) huku akisema kuwa umaarufu wa zao hilo umekuja mara baada ya masoko huria kuanzishwa.

Kisia amepongeza juhudi za serikali katika misimu miwili ya mwaka 2016/2017 na 2017/2018 kwa kutatua suala la kupanda kwa bei ya pembejeo huku akizitaja changamoto katika zao la tumbaku kuwa ni pamoja na kupungua kwa mahitaji ya tumbaku, Kushuka kwa bei ya wastani ya tumbaku, pamoja na Ukubwa wa riba za mikopo.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya zao la tumbaku Tanzania Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya tumbaku Tanzania Dkt Julius Ningu ameitaja mikoa inayolima tumbaku kwa wingi kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Morogoro, Iringa, Ruvuma na Mara huku akiutaja mkoa wa Tabora kuongoza kwa uzalishaji kwa takribani asilimia 50 ya tumbaku yote inayozalishwa nchini.

Alisema kuwa zao la tumbaku lina mchango mkubwa katika pato la Taifa ambapo pato la mkulima limeongezeka kutoka shilingi za kitanzania 2,242,030 mwaka 2011/2012 hadi shilingi 5,982,745 mwaka 2016/2017 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 166.8

Makusanyo ya ushuru wa Halmashauri za Wilaya yameongezeka kutoka shilingi bilioni 10.8 mwaka 2011/2012 hadi shilingi bilioni 14.8 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 37. Huku mapato ya fedha za kigeni yakiwa yameongezeka kutoka dola milioni 302.8 mwaka 2011 hadi dola milioni 343.9 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 14.

Wednesday 6 June 2018

MULTICHOICE TANZANIA YAPONGEZWA KWA MCHANGO WAO KATIKA KUTANGAZA FILAMU ZA KITANZANIA

 Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harison Mwakyembe akimkabidhi Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana tuzo maalum iliyotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania kutambua mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya filamu hapa nchini. Hiyo ilikuwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Suzan Mlawi na mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Prof. Frowin Nyoni.


ARSENAL YASAJILI MZEE MWINGINE AMRI WA MIAKA 34..


Arsenal imemsajili beki mkongwe wa pembeni, Stephan Lichtsteiner kutoka Juventus  

WASIFU WA LICHTSTEINER:  

Umri: Miaka 34
Nafasi: Beki wa kulia
Klabu alizochezea: Grasshoppers (2001-2005), Lille (2005-2008), Lazio (2008-2011), Juventus (2011-2018), Arsenal (2018-)
Idadi ya mechi za klabu: 565
Mabao: 29; Pasi za Mabao: 46
Mechi za kimataifa
(Uswisi): 99
Mataji: Serie A Mara 7
(kila msimu kuanzia 2011 hadi 2018), Coppa Italia Mara 5;  (2009, 2015, 2016, 2017, 2018),Super Cup ya Italia Mara 4; (2010, 2013, 2014, 2016), 2002/2003 Ligi ya Uswisi

KLABU ya Arsenal imethibitisha kumsajili beki mkongwe wa pembeni, Stephan Lichtsteiner kama mchezaji huru kutoka Juventus
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uswisi anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Washika Bunduki hao tangu kuwasili kwa kocha Unai Emery aliyechukua nafasi ya Mfaransa, Arsene Wenger.
Emery ameiambia tovuti ya klabu kwamba: "Stephan analeta uzoefu mkubwa na uongozi katika kikosi chetu. Ni mchezaji mwenye ubora mkubwa mtazamo mzuri na mwenye maamuzi. Stephan atatuimarisha ndani na nje ya Uwanja,".
Pamoja na Lichtsteiner, mwenye umri wa miaka 34 kushinda mataji ya Serie A katika misimu yake yote saba ya kuwa na klabu hiyo ya Turin, lakini anahamia London ambako anavaa jezi namba 12. 
Amecheza mechi zaidi ya 250 akiwa na Juve na anatarajiwa kuichezea mechi ya 100 timu yake ya taifa, Uswisi - ambayo amekuwa Nahodha wake tangu mwaka 2016 - katka mchezo wa kirafiki Ijumaa dhidi ya Japan.
Kama hatacheza mechi hiyo, Lichtsteiner atafikisha mechi zake 100 Uswisi katika mchezo wa kwanza wa Kombe l Dunia dhidi ya Brazil Juni 17.
Arsenal haijasema Lichtsteiner amesaini mkataba wa muda gani ingawa imesema atajiunga na Wahika bunduki hao atakapomaliza mkataba waje Juventus mwezi huu.
Lichtsteiner atashindana na Hector Bellerin kugombea namba katika beki ya kulia kwenye kikosi cha Emery. 

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube