Klabu ya Manchester United imethibitisha kumsajili kiungo wa Brazil, Frederico Rodrigues de Paula Santos, kwa uhamisho wa paundi £52m kutoka Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine.
Fred ambaye amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil katika mashindano ya kombe la dunia mwaka huu huko Urusi, amesaini mkataba wa miaka mitano.
Usajili huo wa Fred kujiunga na Man United umekuwa wa kwanza kwa Kocha Jose Mourinho katika msimu huu wa majira ya joto tangu kumalizika kwa ligi kuu England.
Mshambuliaji huyo alihusika kwenye mtanange wa kirafiki kati ya Brazil dhidi ya Croatia ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mchezaji huyo ameondoka Shakhtar baada ya kuitumikia kwa takribani miaka mitano tangu alipojiunga nayo mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment