Arsenal imemsajili beki mkongwe wa pembeni, Stephan Lichtsteiner kutoka Juventus PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Arsenal imethibitisha kumsajili beki mkongwe wa pembeni, Stephan Lichtsteiner kama mchezaji huru kutoka Juventus.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uswisi anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Washika Bunduki hao tangu kuwasili kwa kocha Unai Emery aliyechukua nafasi ya Mfaransa, Arsene Wenger.
Emery ameiambia tovuti ya klabu kwamba: "Stephan analeta uzoefu mkubwa na uongozi katika kikosi chetu. Ni mchezaji mwenye ubora mkubwa mtazamo mzuri na mwenye maamuzi. Stephan atatuimarisha ndani na nje ya Uwanja,".
Pamoja na Lichtsteiner, mwenye umri wa miaka 34 kushinda mataji ya Serie A katika misimu yake yote saba ya kuwa na klabu hiyo ya Turin, lakini anahamia London ambako anavaa jezi namba 12.
Amecheza mechi zaidi ya 250 akiwa na Juve na anatarajiwa kuichezea mechi ya 100 timu yake ya taifa, Uswisi - ambayo amekuwa Nahodha wake tangu mwaka 2016 - katka mchezo wa kirafiki Ijumaa dhidi ya Japan.
Kama hatacheza mechi hiyo, Lichtsteiner atafikisha mechi zake 100 Uswisi katika mchezo wa kwanza wa Kombe l Dunia dhidi ya Brazil Juni 17.
Arsenal haijasema Lichtsteiner amesaini mkataba wa muda gani ingawa imesema atajiunga na Wahika bunduki hao atakapomaliza mkataba waje Juventus mwezi huu.
Lichtsteiner atashindana na Hector Bellerin kugombea namba katika beki ya kulia kwenye kikosi cha Emery.
No comments:
Post a Comment