Baada ya kuiondosha Kariobangi Sharks FC katika michuano ya SportPesa Super Cup, klabu ya Simba itakutana na wababe wa Yanga, Kakamega HomeBoyz, kesho Alhamis kwenye Uwanja wa Afraha.
Michuano hiyo inayoendelea mjini Nakuru itakuwa inazikutanisha Simba na Kakamega kwenye mchezo huo wa hatua ya nusu fainali itakayoanza majira ya saa 9 kamili mchana.
Kakamega walifuzu kufika fainali baada ya kuifunga Yanga katika ufunguzi wa pazia la mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-1.
Wakati huo Simba nayo ilitinga nusu fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penati na kushinda 3-2 dhidi ya Kariobangi Sharks FC.
Jumla ya timu 4 zimetinga nusu fainali ambazo ni Simba SC (Tanzania), Gor Mahia FC (Kenya), Singida United (Tanzania) na Kakamega HomeBoyz (Kenya).
No comments:
Post a Comment