BREAKING

Thursday, 12 October 2017

WAAJIRI WA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI JIJINI MWANZA WALAUMIWA.


Mkufunzi wa mafunzo kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani katika Kata ya Buhingwa Jijini Mwanza, akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo hii leo. Mafunzo hayo yafanyika kwenye ukumbi kwa kanisa la AICT Buhingwa kuanzia jana na yatafikia tamati kesho Oktoba 12,2017.

Baadhi ya waajiri wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wameelezwa kuwa kikwazo cha kuwaruhusu watoto hao kupata elimu ya utambuzi yanayotolewa na shirika la WoteSawa.
Mratibu wa shirika hilo linalotetea haki na maslahi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani, Cecilia Nyangasi ameyasema hayo hii leo wakati wa mafunzo kwa watoto wafanyakazi katika Kata ya Buhongwa jijini hapa.

“Waajiri wamekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu wengi wao wanadhani kwamba tunakuja kuwapotosha watoto wao”. Alisema Nyangasi na kubainisha kwamba shirika la WoteSawa linatoa elimu ya kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao kisheria, wajibu wao kazini pamoja na elimu ya afya ya uzazi ili kuondokana na mimba za utotoni.

Nyangasi alisema baada ya mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia jana, itaundwa kamati ya watoto wafanyakazi wa nyumbani Kata ya Buhongwa kama ilivyofanyika kwenye Kata za Nyakato, Mecco, Isamilo, Pasiansi, Kirumba na Mkuyuni ambapo jukumu kubwa la kamati hizo ni kuwa mabalozi wa watoto wengine ambao hawakufikiwa na mafunzo hayo.

Suzana John na Lugwisha Zakaria ambao ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyojumuisha watoto 47 katika Kata hiyo ya Buhongwa, wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kutambua haki zao kisheria na pia wajibu wao kama waajiriwa.
Mwanasheria Joseph ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo
Mkufunzi wa mafunzo hayo akifafanua jambo
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza akiuliza swali
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza akiuliza swali
Washiriki wa mafunzo hayo katika Kanda ya Buhongwa Jijini Mwanza
Washiriki wa mafunzo hayo katika Kanda ya Buhongwa Jijini Mwanza
Mratibu wa WoteSawa, Cecilia Nyangasi (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo
Afisa kutoka shirika la WoteSawa la Jijini Mwanza
Suzana John, mshiriki wa mafunzo hayo

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube