BREAKING

Tuesday, 3 October 2017

KOCHA CARLO ANCELOTTI AAMUA KUJIPA LIKIZO NDEFU YA MWAKA KUTOJIHUSISHA NA UKOCHA


Wik moja tangu atimuliwe na klabu ya Bayern Munich kufuatia matokeo mabaya katika mfululizo wa mechi za timu hiyo, kocha Carlo Ancelotti ametangaza kuwa atakwenda mapumzikoni ambapo hatafanya kazi ya kufundisha soka kwa kipindi cha miezi kumi.

Kocha huyo ametoa kauli hiyo huku kukiwa na uvumi kwamba klabu ya AC Milan inataka kumrejesha kufuatia tetesi za kuwa huenda ikaachana na kocha wake wa sasa Vincenzo Montella anayelaumiwa kwa matokeo mabaya katika ligi kuu nchini Italia.

Ancelotti ambaye amesisitiza kuwa hatafundisha soka kwa miezi kumi, tayari ameviongoza vilabu kadhaa vya ulaya kutwaa uchampioni katika mashindano mbalimbali vikiwemo Parma, Juventus, AC 
Milan, Chelsea, PSG, na Real Madrid.








No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube