KIKOSI cha Simba kimerejea asubuhi ya leo mjini Dar es Salaam kwa ndege maalum ya kukodi kutoka kisiwani Zanzibar, ambako waliweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga kesho. Simba wameteremkea Uwanja wa ndege wa zamani, maarufu kama Terminal One na moja kwa moja kuelekea katikati ya Jiji, ambako wataweka kambi katika hoteli ya Serena, tayari kwa mchezo wa kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba walioonekana watulivu mno wakati wanawasili Terminal One, walikuwa wakitoka ndani na moja kwa moja kupanda basi la timu lililokuwa hapo linawasubiri, huku kukiwa na ulinzi mkali wa ‘makomandoo’ wa timu.
Friday, 27 October 2017
NI SIMBA NA YANGA UWANJA WA UHURU NANI KUIBUKA MBABE KWA MWENZAKE, SIMBA WAREJEA KUTOKA PEMBA.....
KIKOSI cha Simba kimerejea asubuhi ya leo mjini Dar es Salaam kwa ndege maalum ya kukodi kutoka kisiwani Zanzibar, ambako waliweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga kesho. Simba wameteremkea Uwanja wa ndege wa zamani, maarufu kama Terminal One na moja kwa moja kuelekea katikati ya Jiji, ambako wataweka kambi katika hoteli ya Serena, tayari kwa mchezo wa kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba walioonekana watulivu mno wakati wanawasili Terminal One, walikuwa wakitoka ndani na moja kwa moja kupanda basi la timu lililokuwa hapo linawasubiri, huku kukiwa na ulinzi mkali wa ‘makomandoo’ wa timu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment