Beki wa Barcelona Gerard Pique amesema atastaafu soka ya kimataifa kabla ya Kombe la Dunia iwapo ataendeleza kukosolewa kwa kuunga mkono kura ya maoni ya uhuru wa jimbo la Catalonia.
Barcelona walilaza Las Palmas 3-0 katika mechi iliyochezewa uwanja usio na mashabiki Jumapili baada ya maandamano kukumba jiji la Barcelona.
Wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Columbia mjini Murcia, mji ulio kusini mashariki mwa Uhispania, alizomewa na mashabiki wanaopinga uhuru wa Catalonia.
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos ameingilia kati na kuwataka mashabiki wamheshimu mwenzake huyo katika timu ya taifa.
KWA PICHA ZAIDI BONYEZA HAPA......
No comments:
Post a Comment