Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika moja ya shule ya msingi akiwa katika ziara ya kutambua changamoto na kuzifanyia kazi ili ziwe na ubora kama shule za watu binafsi na kuongeza ufaulo kwa wanafunzi wanasoma katika shule hizo.
Mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa darasani na wanafunzi wa shule ya msingi Kibwabwa iliyopo kata ya Kitwiru manispaa ya IringaMbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kuzitambua changamoto za shule za msingi.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalam mkoa
wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za
manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza
kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.
Akizungumza mara baada ya
kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule
ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto
nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.
“Nimejionea mwenyewe changamoto
zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi
yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati
Kabati alisema kuwa
atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama
nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi za Azimio na Kigonzile ambazo
kwa sasa zinaubora kama shule za watu binafsi.
“Kwa kweli wadau wamekuwa
wakinisaidia kufanikisha swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa
manispaa ya Iringa ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama
shule za watu binafsi” alisema kabati
Aidha Kabati aliwataka
viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa kuzitembelea shule hizo mara kwa
mara ili kutatua matatizo haya mapema kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio
maana miundombinu imeharibika kwa kiasi kikubwa.
“Viongozi wengi tunashinda
sana maofisini kuliko kwenda kuyatembelea maeneo yenye changamoto kama hizi za
shule za msingi za manispaa ya Iringa kwasababu ukitembelea maeneo yenye
changamoto mara kwa mara inakuwa kazi rahisi kuzitafutia ufumbuzi mapema”
alisema Kabati
Kabati alisema kuwa shule
nyingi za msingi manispaa ya Iringa zilijengwa miaka 1980 ndio maana saizi
miundombinu imeharibika kutokana na kutokarabatiwa mara kwa mara na kusababisha
kuendelea kuharibika kwa kuwa hakuna mikakati ya makusudi ya kukarabati shule
hizo.
Kabati aliwaomba wananchi na
wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano wa kutosha ilikufanikisha azma ya
kuzikarabati shule hizo na kuacha kuangalia Itikadi ya vyama vya siasa kwa kuwa
maendeleo hayana siasa
.
Naye mwenyekiti wa kamati ya
shule ya msingi Kibwabwa Isumael Mlenga alimpongeza mbunge huyo kwa kazi
anayoifanya ya kusaidia kukarabati shule za msingi za manispaa ya Iringa ni
jukumu kubwa analolifanya kwa wanairinga.
“Ni wabunge wachache wenye
moyo kama wa Ritta Kabati hivyo tunapaswa kuendelea kumuunga mkono kwenye kazi
anazozifanya kwa maendeleo ya watoto wetu wanaosoma katika shule hizo
zinazokarabatiwa na mbunge huyo” alisema Mlenga
Karumerita Mbuta,Zubeiry
Mlowela na Romana Lutenga ni wajumbe wa kamati ya shule ya Kibwabwa
walimpongeza mbunge huyo kwa ziara zake anazozifanya kuzitambua Changamoto
zilizopo mashuleni hasa kwenye shule za msingi hivyo tunaomba ziara zako ziwe
na matunda kwa kuboresha miundombinu ya shule ulizotembelea.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
No comments:
Post a Comment