Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ataifuata timu yake mjini Shinyanga.
Yanga inaondoka leo kwenda mjini Bukoba ikipitia Mwanza kwenda kuivaa Kagera Sugar.
Ngoma na Thabani Kamusoko wanaachwa Dar es Salaam ili kuendelea na matibabu kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini Ngoma, atakwenda Shinyanga kwa kuwa atakuwa amerejea katika hali yake.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema baada ya mechi ya Jagera, watakwenda Shinyanga kuivaa Stand United ambako Ngoma ataungana nao.
"Wakati tukiwa Shinyanga tutaungana na Ngoma. Daktari amesema atakuwa amerejea katika hali nzuri," alisema.
No comments:
Post a Comment