BREAKING

Friday, 27 October 2017

MAKAMU WA RAIS KUWA MGENI RASMI KWENYE MATEMBEZI YA HISANI JIJINI DAR ES SALAAM

Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank M, linawakaribisha wananchi wote kwenye Matembezi ya Hisani 2017 yanayolenga kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuwasomesha wauguzi wakunga ili kupata ujuzi wa kutoa huduma bora wakati wa kujifungua. 

Matembezi hayo yatafanyika Novemba 04, 2017 katika Viwanja vya Green Grounds Oysterbay Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa nne asubuhi (12:30 – 4:00 asubuhi).

Mgeni Rasmi katika matembezi hayo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ambapo yanaambatana na kauli isemayo “Karibuni Tutembee Pamoja,  Tusomeshe Wauguzi  Wakunga Zaidi, kwa Uzazi Salama”.

Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wanahimizwa kuungana na Amref katika juhudi za kuongeza idadi ya wauguzi wakunga wenye ujuzi kwa kununua tiketi kwa shilingi 25,000 ambapo tiketi hiyo itaambatanishwa na tisheti matembezi hayo.
Tayari tiketi zinapatikana katika ofisi za Amref zilizopo Upanga karibu na ubalozi wa Japani Jijini Dar es salaam lakini pia waweza kupiga simu nambari 0767 30 30 14 ama 0658 00 67 07 kwa ufafanuzi zaidi.

Aidha malipo kwa ajili ya kupata tiketi yanafanyika kupitia nambari ya M-PESA 0762  223  348 ama kupitia Bank Account nambari 02 50 02 73 31 BANK M

Tembelea ukurasa wa Facebook wa Amfref  https://www.facebook.com/AMREFHealthAfricaTZ/# ama tovuti www.amref.org kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube