BREAKING

Friday, 27 October 2017

NI SIMBA NA YANGA UWANJA WA UHURU NANI KUIBUKA MBABE KWA MWENZAKE, SIMBA WAREJEA KUTOKA PEMBA.....



KIKOSI cha Simba kimerejea asubuhi ya leo mjini Dar es Salaam kwa ndege maalum ya kukodi kutoka kisiwani Zanzibar, ambako waliweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga kesho.   Simba wameteremkea Uwanja wa ndege wa zamani, maarufu kama Terminal One na moja kwa moja kuelekea katikati ya Jiji, ambako wataweka kambi katika hoteli ya Serena, tayari kwa mchezo wa kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba walioonekana watulivu mno wakati wanawasili Terminal One, walikuwa wakitoka ndani na moja kwa moja kupanda basi la timu lililokuwa hapo linawasubiri, huku kukiwa na ulinzi mkali wa ‘makomandoo’ wa timu.

WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (pichani juu), amewaomba radhi wananchi kufuatia kukatika kwa umeme nchi nzima Oktoba 25 na 26, 2017 kulikosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa.
Dkt. Kalemani amabye alikuwa mjini Dodoma akishiriki vikao vya kamati za bunge, alilazimika kusafiri mapema leo asubuhi Oktoba 26, 2017 kuja jijini Dar es Salaam ili kufuatilia juhudi za kurekebisha tatizo hilo.
"Ndugu wananchi hali ilivyotokea sisi kama Shirika la TANESCO na Serikali tunawataka radhi wananchi kwa matatizo yaliyotokea lakini niseme tu kwamba kuna hatua madhubuti zinazochukuliwa hivi sasa kurekebisha hali hiyo ili wananchi muendelee kupata umeme wa uhakika." Alisema Dkt. Kalemani katika taarifa yake kwa wananchi aliyoitoa makao makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam baada ya ziara yake ya kutembelea kituo cha udhibiti cha Gridi ya Taifa, (GCC), kilichoko Ubungo na kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi1 jijini  Dar es Salaam.

Taarifa za awali zilieleza kuwa kukatika kwa umeme kulisababishwa na "Gridi kuchomoka" Oktoba 25, 2017 majira ya saa 10;08 alfajiri na kurejea saa 12:09 asubuhi ambapo umeme ulirejea mikoa yote isipokuwa Zanzibar, ingawa juhudi za mafundi wa TANESCO ziliwezesha umeme kurejea Zanzibar majira ya saa 1 asubuhi.
Hata hivyo tatizo hilo lilirejea tena majira ya saa 12:30 jioni siku hiyo hiyo ya Oktoba 25, 2017, ambapo takriban mikoa yote iliathirika. Umeme ulirejea tena majira ya saa 3 usiku lakiji ilipofika Oktoba 26, 2017 majira ya saa 12:03 tatizo hilo likajirudia tena na kuathiri takriban mikoa yote ikwiemo Zanzibvar.

"Nimekuja kutoka Dodoma ili kuona nini kimetokea, nini kimesababisha na hatua gani za haraka zichukuliwe ili kuondoa tatizo hilo hii ndio hasa dhamira ya safari yangu." Alisema Dkt. Kalemani baada ya kufika kwenye kituo cha udhibiti Gridi ya Taifa, Ubunmgo.
Lakini niwapongeze TANESCO kwa kutoa taarifa mapema kwa wananchi kuwajulisha kuhusu tatizo hilo, alisema.
Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema, chanzo cha tatizo ni pamoja na mfumo wenyewe (GCC) na bado unafanywiwa marekebisho na taratibu zinaendelea, na kule Kinyerezi kuna mashine moja haifanyi kazi nayo inafanyiwa marekebishiom ikiwa ni pamoja na valvu moja iliyoharibika nayo pia inafabnyiwa kazi.
"Gridi ya taifa imerejea tangu jana usiku (Oktoba 25), na umeme unapatikana nchi nzima lakini hata hivyo yapo maeneo machache ambayo hayapati umeme wa kutosha kwa sababu mtambo mmoja wa Ubungo namba mbili wenye jumla ya megawati 129 haujaanza kufanya kazi na nimeelekeza wataalamu wafanye kazi usiku na mchana na wamenihakikishia kufikia saa 5 asubuhi kesho  (Oktoka 27), mtambo huo utaanza kufanya kazi na umeme utarejea katika hali yake ya kawaida." Alibainisha.

Dkt. Kalemani akiwa kwenye kituo cha udhibiti wa Gridi ya Taifa (GCC), Ubungo jijini Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji (Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kushoto), akimpatia maelezo Waziri Dkt. Kalemani alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi 1 jijini Oktoba 26, 2017. Wakzanza kulia ni NJaibu Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Juliana Palagyo
Meneja Mwandamizi wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji, Mhandisi Costa Rubagumya akifafanua jambo.
Meneja wa udhibiti  ifumo ya Gridi ya Taifa (Protection), Mhandisi Izahaki Mosha, akimfafanulia Waziri Dkt. Kalemani (kushoto).
Dkt. Kalemani (kushoto), akiwa kwenye chumba cha udhibiti cha Kinyerezi 1 akifafanua jambo.

WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE


Watafiti, Dk.Beatrice Lyimo (wa tano kushoto) na Bestina Daniel (wa pili kulia), kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),wakiwakabidhi mbegu bora ya mihogo Wanakikundi cha Chapakazi katika  Kijiji cha Kalebezo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo. 

 Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala (kulia), akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akizungumza.
 Mtafiti, Dk.Beatrice Lyimo kutoka COSTECH, akizungumzia kuhusu mradi huo wa mbegu bora
 Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura (mwenye mbegu), akitoa mafunzo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hiyo ya mhogo aina ya Mkombozi iliyozalishwa kitaalamu. 
Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura, akielekeza namna ya upandaji wa mbegu ya viazi lishe katika kijijini cha Msenyi
 Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala, akipanda mbegu hiyo katika shamba darasa kijijini Kalebezo.



 Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akipanda mbegu ya mhogo.
 Ofisa Ugani, Jonas Kamugisha akipanda mbegu ya mhogo.
 Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kalebezo, Juster Nkuna akipanda mbegu ya mhogo.
 Mbegu ya mhogo ikishushwa kutoka kwenye gari tayari kwa uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Kalebezo.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapajembe wa Kijiji cha Msenyi, Josia Kagwingi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe katika kijiji hicho. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kikundi hicho, Mariana Mariko na kulia ni mwanakikundi, Zabia Emanuel.


Mkulima wa Kijiji cha Msenyi, Martin Tibenda akipanda mbegu ya viazi lishe katika uzinduzi wa shamba darasa.

Na Dotto Mwaibale, Biharamulo Kagera.

WAKULIMA wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa kuwapelekea mbegu bora ya migomba,mihogo na viazi lishe ambayo itapandwa katika mashamba darasa na kusambazwa kwa wakulima wengine katika wilaya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.

"Kwa niaba ya Ofisa Kilimo wa wilaya napenda kuishukuru COSTECH kwa kutuletea mbegu hizo katika wilaya yetu hasa baada ya kuona changamoto tuliyokuwa tukikabiliana nayo ya magonjwa ya mihogo kama batobato" alisema Ngawagala.

Ngawagala alisema msaada huo hautapotea bure kwani watahakikisha wanayahudumia vizuri mashamba darasa hayo likiwemo la mihogo lililopo katika Kijiji Kalebezo na lile la viazi lishe lililopo Kijiji cha Msenyi ambayo yamezinduliwa na kuhudhuriwa na wakulima kutoka vikundi vya Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo na Chapajembe cha Kijiji cha Msenyi vyote vya wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Chapakazi, Thadeo Kibuka alisema mbegu hiyo waliyoletewa itakuwa mkombozi wao kwani kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya kupata mazao yenye magonjwa kutokana na kukosa mbegu bora na ukame.

"Tutahakikisha shamba ili tunalo lizindua leo hii kwa msaada wa COSTECH na OFAB linakuwa la mfano wa kuzalisha mbegu bora katika wilaya hii" alisema Kibuka.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Mtafiti Dk. Beatrice Lyimo alisema COSTECH kwa kushirikiana na OFAB wanaendesha mradi huo ili kuhakikisha kuhakikisha matokeo mazuri ya kazi za tafiti yanawafikia wakulima na kupata chakula cha kutosha.


Alisema COSTECH ndio mshauri mkubwa wa serikali katika masuala ya kilimo cha kitafiti hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha tafiti zinazofanyika nchini zikiwafikia walengwa ili waweze kufanya vizuri katika kilimo.


Dk. Lyimo aliwataka wakulima hao kwa kushirikiana na maofisa ugani kuyatunza mashamba darasa hayo ili kupata mbegu nyingi za mazao hayo na kuzisambaza kwa wakulima wengine.

Ofisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis  Baraka alisema mkoa huo umepata bahati kubwa kwa kupelekewa mbegu hizo katika wilaya tano ambapo katika kila wilaya vijiji viwili vilichaguliwa kuanzisha shamba darasa la mbegu ya mhogo na migomba na viazi lishe kutegemea uhitaji wa zao gani katika kijiji husika.

"Tuna bahati kubwa kuletewa mradi huu katika mkoa wetu hivyo tusiwaangushe hawa wenzetu tuwe wa mfano tuyatunze haya mashamba ili tupate matokeo mazuri" alisema Baraka.


Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura amewataka wakulima hao kutambua kuwa mbegu hizo za mihogo walizokabidhiwa zinatunzwa vizuri kwani zinauwezo wa kutoa tani 32 za mhogo kwa ekari moja na kwa viazi lishe zinatoa tani 7 hadi 9 kwa ekari tofauti na mbegu za zamani ambazo hazina tija.

Mashamba darasa ya mbegu bora za Mihogo,Viazi lishe na Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa yaliyoanzishwa katika mkoa huo yanajumuisha wilaya tano za Mkoa wa Kagera baada ya COSTECH na OFAB kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo wa wilaya hizo na  kata zote ikiwa na lengo la kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao yao kwa tija na kuachana na kilimo kisicho bora na tija.

MAKAMU WA RAIS KUWA MGENI RASMI KWENYE MATEMBEZI YA HISANI JIJINI DAR ES SALAAM

Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank M, linawakaribisha wananchi wote kwenye Matembezi ya Hisani 2017 yanayolenga kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuwasomesha wauguzi wakunga ili kupata ujuzi wa kutoa huduma bora wakati wa kujifungua. 

Matembezi hayo yatafanyika Novemba 04, 2017 katika Viwanja vya Green Grounds Oysterbay Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa nne asubuhi (12:30 – 4:00 asubuhi).

Mgeni Rasmi katika matembezi hayo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ambapo yanaambatana na kauli isemayo “Karibuni Tutembee Pamoja,  Tusomeshe Wauguzi  Wakunga Zaidi, kwa Uzazi Salama”.

Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wanahimizwa kuungana na Amref katika juhudi za kuongeza idadi ya wauguzi wakunga wenye ujuzi kwa kununua tiketi kwa shilingi 25,000 ambapo tiketi hiyo itaambatanishwa na tisheti matembezi hayo.
Tayari tiketi zinapatikana katika ofisi za Amref zilizopo Upanga karibu na ubalozi wa Japani Jijini Dar es salaam lakini pia waweza kupiga simu nambari 0767 30 30 14 ama 0658 00 67 07 kwa ufafanuzi zaidi.

Aidha malipo kwa ajili ya kupata tiketi yanafanyika kupitia nambari ya M-PESA 0762  223  348 ama kupitia Bank Account nambari 02 50 02 73 31 BANK M

Tembelea ukurasa wa Facebook wa Amfref  https://www.facebook.com/AMREFHealthAfricaTZ/# ama tovuti www.amref.org kwa taarifa zaidi.

Monday, 16 October 2017

UHURU FM WALIPOLIAMSHA DUDE JANA WENYE VIWANJA VYA MWEMBEYANGA, TEMEKE, KATIKA TAMASHA LA 'GUSA MAISHA YAKE' KUMUENZI BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU NYERERE


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Juma Kiroboto, maarufu Juma Nature, akisababisha jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
Mwanamuziki wa muziki Isha Mashauzi akipagawisha mashabiki, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kweneye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwa jukwaani, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Mwanamuziki wa muziki wa Singeli Dula Makabila akiwapandisha mori mashabiki wake walioamua kupanda  jukwaani na kuonyesha uhodari wao wa kucheza muziki huo, katika Tamasha la 'Gusa Maisha yao' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandaliwa na Uhuru FM katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Dansa wa Dula Makabila akionyesha umahiri wake wa kucheza Singeli
Vijana wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakishambulia jukwani
Msanii wa muziki wa Singeli akionyesha umahiri wake wa kuteka mashabiki
Wachezaji wa timu zilizoshiriki kunogesha tamasha hilo wakichuana vikali kuwania mpira. 
Wachezaji wa timu zilizoshiriki kunogesha tamasha hilo wakichuana vikali kuwania mpira.
Mchuano mkali wa soka kwenye tamasha hilo
Wanamuziki wa bendi ya TOT Plus wakishiriki kunogesha tamasha hilo. Kulia ni kiongozi wao Abdul Misambano
Mcheza shoo wa TOT Plus Gabriel Romao maarufu kwa jina la Matukutuku akionyesha uwezo wake jukwaani
Matukutuku wa TOT akicheza hadi kwa kichwa chini kukata kiu ya machabiki kwenye tamasha hilo
KatamuTamu wa TOT Plus akionyesha uwezo wake wa kucheza shoo jukwaani
Mtangazaji wa Uhuru FM Kigwa akichangasha jukwaa
"Mashabiki piga keleeeee" Kigwa akihamasisha uchangamfu kabla ya Vijana Jazz kupanda jukwaani
Waimbaji wa Vijana Jazz wakiimba kwa hisia kali kudhihirisha kuwa muziki wa dansi bado una nafasi na mashabiki wake wapo.
Kijana Saamata Hussein wa Vijana Jazz akionyesha umahiri wa 'kukaanga chips' jukwani
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Dansi, Anna Mwaole akionyesha bado wamo, wakati akiimba na bdndi hiyo ya Vijana jazz. Anasema yeye ni Kongoro la supu lisiloisha utamu na pia ni kisu cha mgema
Cosmas Adilian na Mohammed kandera wakionyesha umahili wa kupuliza tarumpeta katika bendi hiyo ya Vijana Jazz
Shabiki akionesha 'kuguswa maisha yake' na burudani zilizokuwa zikimimika kutoka makundi mbalimbali kwenye tamasha hilo
Mwimbaji wa Mwenge Jazz Shukuru Majaliwa akionyesha hisia zake wakati akiimba kibao cha siku nyingi cha Zena.
Mwenge Jazz wakishambulia jukwaa
Mwimbaji wa Mwenge Jazz akikoleza kwa kusakata muziki jukwaani
Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akifurahia jambo na mwenzake wakati wa tamasha hilo, kabla ya kuanza utambulisho wa baadhi ya watangazaji wa kituo hicho cha radio
Mtangazaji waa Kipindi cha Uhuru Fleva ambacho ndicho kilikuwa mwenyeji wa tamasha hilo, Saidi Ambua, akimtambulisha Mtangazaji Steven Mhina Dungumalo
Akiendela kumtambulisha Mhina
Mhina akisalimia
Mhina akazungumza kisha utambulisho ukaendelea kwa wengine
Mwajuma Yamka wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba akiwa na Meneja rasiliamali watu wa Uhuru FM Paul Mg'ong'o kwenye tamasha hilo
Sabrina Kado akitoka kupoza koo na Wanamuziki wenzake
Ambua akiteta jambo na mwanamuziki nguli Hussein Jumbe kwenye tamasha hilo
Angel Akilimali akiwa na Mwanamuziki Isha Mashauzi kwenye tamasha hilo
Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa na Hussein Jumbea na Isha Mashauzi
Paul Mng'ong'o akisalimiana na Kiongozi wa FM Academia Nyoshi El Saadat
Ma DJ John Dilinga na Fast Edie wakiwa kwenye tamasha hilo
Msondo Ngoma wakiwa jukwaani kwenye Tamasha hilo
Romanus Mng'ande aka Romario akifanya vitu vyake na Bendi ya Msondo
Pince Muumini Mwinjuma akiwa na Wanamuziki wake kwenye tamasha hilo
Mwanamama akitafuta wateja wa Ming'oko kwenye tamasha hilo la Gusa Maisha yao
Baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru FM kwenye tamasha hilo
Wananchi waliohudhuria tamasha hilo la 'Gusa maisha yao' wakifurahi kuonyesha kuguswa na tamasha hilo ambalo lilikuwa mahsusi kumueenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere. 
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube