BREAKING

Thursday 3 August 2017

MULTICHOICE WAZINDUA MSIMU MPYA WA LIGI UINGEREZA

 Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania MAHARAGE CHANDE akionyesha umahiri wake wa kupiga dana dana, wakati wa hafla ya kuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza,kupitia DSTV.
 Mkuu wa Masoko wa Multichoice Tanzania mwenye mpira Alpha Joseph, akiwa katika pozi wakati wa hafla ya kuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza

Multichoice Tanzania kupitia kingíamuzi cha DSTv imezindua rasmi Msimu mpya wa Sokaî wakitumia kampeni mpya ya ìFull Vyenga Bila Chengaî.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande aliongoza zoezi hilo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye ofisi zao jijini Dar es Salaam.

Wakati wa uzinduzi huo Maharage ameeleza kuwa watapunguza bei ikiwa ni pamoja na kuuza kingíamuzi cha Sh 79,000 na kinakuwa kingíamuzi nafuu zaidi chenye burudani ya uhakika ya soka.

Aidha ameel;eza zaidi kuwa wapenzi wa soka watatazama burudani hiyo,  kupitia king'amuzi cha DSTv chenye ubora mkubwa na wataweza kuona kila matukio, ambapo amesema pia Kingíamuzi hicho kitaonyesha matangazo yanayorushwa katika lugha ya Kiswahili ili kuwapa watu nafasi ya kuelewa zaidi

Naye Mkuu wa Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Joseph ,amesema kuwa ameeleza namna ambavyo wamekuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kusaidia Watanzania wengi kuburudika na soka katika ligi mbalimbali kama Ligi ya Uingereza, Ligi ya  La Liga ya Hispania, Serie A ya Italia, League 1 ya Ufaransa na ligi nyingine mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube