BREAKING
ROSE MHANDO :MSAMA NI BABA KWANGU ACHENI KUNIGOMBISHA NAYE.   UPANDIKIZAJI WA MENO BANDIA KWA NJIA YA KISASA MUHIMBILI MLOGANZILA 45 KUNUFAIKA NA HUDUMA    UTEKAJI WA WATOTO MKUU WA MKOA WA MBEYA JUMA HOMERA AWATAKA WANAFUNZI WA HOLY LAND PRE- & PRIMARY SCHOOL KUKATAA LIFTI   MSAMA ANG'AKA WAIMBAJI WA IN JILI KUPOTOKA MAADILI   DCEA YAFANIKIWA OPERESHENI DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA JAHAZI DAWA ZA KULEVYA   NAIBU WAZIRI MKUU AKARIPIA UZEMBE TANESCO   MHE. RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZA NA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING    MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI CHINA..   RAIS SAMIA NCHINI KENYA-ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI   RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA-KENYA    Blogger Tips and Tricks & Blogger Templates

Wednesday, April 09, 2025

Wednesday, 2 August 2017

WATEJA WA DSTV WANAKULA KUKU KWA MRIJA WAULA MULTICHOICE , ZAWADI ZAMIMINIKA ZA VING'AMUZI


 

Wateja 76 wa DStv wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika promosheni inayoendelea ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa DStv anapata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa mangalau miezi miwili mfululizo.

Kati ya washindi hao 25 wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya DStv Explora ambavyo ni ving’amuzi vya kisasa kuliko vyote hapa nchini. Washindi watatu wamejishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 184,000) cha mwezi mmoja, wengine watatu Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 122 500), huku washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 82,250), 10 kifurushi cha Famili (42,900) na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,975.

 

Promosheni hii inaendelea kwa muda wa miezi miwili itatoa washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo vifurushi vya muda wa matangazo, ving’amuzi, pamoja na zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar kwa washindi wawili pamoja na familia zao.

Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza leo hii katika ofisi za Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa Zaidi ya wateja elfu 10 wameshiriki kwenye droo hiyo  hii ikionyesha muitikio mkubwa wa wateja.

Pia amebainisha kuwa washindi waliopatikan katika droo ya kwanza wametoka kila pembe ya nchi ikiwemo Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Morogoro.

Amewataka wateja wa DStv kuendelea kulipia ving’amuzi vyao kwani bado droo moja kubwa ya mwisho ambapo kuna wateja wawili watakaoshinda safari ya kutalii Zanzibar pamoja na familia zao.

Amesema promosheni hiyo haina ugumu wa kushiriki kwani anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia kifurushi chochote kile cha DStv na kisha kuendelea kutumia huduma hiyo na moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo zitakazochezeshwa kila baada ya wiki mbili. Droo kubwa ya mwisho tarehe 1/9/201


Afisa muandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah (katikati waliokaa)akifuatilia kwa karibu wakati wa droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv ambapo wateja takriban 100 wa DStv walijishindia zawadi mbalimbali. Kulia ni Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo, Wengine ni maafisa wa Multichoice Erick Mosha (aliyesimama) na Leyla Partick

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube