Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Liverpool, John Barnes,akiwasili |
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Liverpool, John Barnes na mchambuzi wa soka husani Ligi ya Uingereza ametua nchini tayari kwa ajili ya kuendesha kliniki ya soka kwa vijana wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Srengeti Boy's.
Sambamba na hilo Barnes pia atahudhuria awamu ya pili ya mashindano maalumu ya kombe la Standard Chartered ambayo yatashirikisha timu tatu kutoka nchiza za Tanzania, Kenya na Uganda.
Mara baada ya kuwasili Barnes amezungumzia ujio wake na jinsi atakavyokutana na vijana wa Serengeti Boy's huku akisifia programu mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na wadau wa soka akibainisha kuwa japo ni mara yake ya kwanza kutua nchini lakini amekuwa akifuatialia maendeleo ya soka hususani Afrika Mashariki, huku akitambua uwepo wa nyota anayecheza soka la kulipwa Ubelgiji Mbwana Samatta, ambapo amesema ili timu zifanye vizuri lazima kuwekeza kwa vijana.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Alfredy Lucas pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Standard Chartered Tanzania wamesema kuwa ujio wa Barnesw una faida nyingi ikiwepo kuwahamasisha vijana pamoja na kuimarisha vipaji vya soka kwa vijana wa Kitanzania
Wamesema kuwa wanaamini kuwa Barnes atatumia ujuzi wake kadri atakavyoweza ili kuwanufaisha vijana wenye vipaji
No comments:
Post a Comment