Kiungo Arturo Vidal akishangilia mbele ya mashabiki wa Bayern Munich usiku wa jana Uwanja wa Emirates, London baada ya kufunga mabao mawili dakika za 50 na 85 katika ushindi wa 5-1 dhidi ya wenyeji, Arsenal kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao mengine ya Bayern iliyoshinda 5-1 pia kwenye mchezo wa kwanza Munich yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 55 kwa penalti, Arjen Robben dakika ya 68 na Douglas Costa dakika ya 78, wakati la Arsenal iliyomaliza pungufu baada ya Laurent Koscielny kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 54, lilifungwa na Theo Walcott dakika ya 20 |
No comments:
Post a Comment