Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mkurugenzi wake, Boniface Wambura imewaomba wadau wa michezo nchini kumwombea dua ya ushindi, Rais wa Heshima wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Leodgar Tenga, ili aweze kushinda nafasi ya ujumbe katika Baraza la FIFA.
Akiwa katika mahojiano maalum na kituo hiki Wambura amesema kuwa itakuwa heshima kubwa iwapo Tenga atapata nafasi hiyo ya ujumbe, kutokana na uwezo wake katika kuendeleza soka.
Wambura amesema hayo huku kesho ikiwa ndio siku mhimu ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa CAF kuadhimisha miaka 60,ya kuzaliwa kwa CAF pamoja uchaguzi wa kumpata rais mpya wa Shirikisho la soka Afrika CAF
Sambamba na hilo Wambura pia ameitakia kila la kheri Zanzibar kupata uanachama wa CAF na FIFA.
No comments:
Post a Comment