BREAKING

Sunday, 31 January 2016

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE LEO MJINI DODOMA

 NG1
Baadhi ya wabunge wakiwasili katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG2
Naibu Spika Mhe Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG3
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Adrew Chenge akiwakiwasilia tayari kuongoza kikao cha Bunge katika Bunge la 11 linaloendelea mjini Dodoma
NG4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt Philip Mpango akiwasilisha hoja ya Serikali ili Bunge lijadili na kuidhinisha Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano
NG5
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Suleiman Jafo akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG7
Waziri wa Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe.Prof Joyce Ndalichako akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG8
Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Naibu wake
Mhe.Annastazia Wambura walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
NG9
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT) Mhe. Zitto Kabwe walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TANZANIA STANDARD NEWSPAPER LIMETED CHAFANYIKA LEO JIJINI DAR Dar es salaam

tsn4
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, Gabriel Nderumaki akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam jana kilichokuwa kinajadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016.Kulia ni Katibu wa baraza hilo, Shafii Mpenda.

tsn1
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
tsn2
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
tsn3
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.

ZIARA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA MAKAO MAKUU YA POLISI

z1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana .
Z2
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.DIGP ni mmoja wa Viongozi waliopitia katika chuo hicho.
Z3
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho Makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba na Brigedia Jenerali Minja.
Z4
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, DIGP Abdulrahman Kaniki akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha ulinzi wa Taifa (NDC) wakati wa ziara ya kimafunzo ya wanafunzi wa chuo hicho katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA UKOMA DUNIANI


UM1 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akiongea an waandishi wa habari (Hawapo Pichani) leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani Kushoto ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba. UM2 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani UM3
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa ukoma na kwa Tanzania Elimu zaidi itatolewa ili kupambana na ugonjwa huu.
UM4 Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani UM5
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia picha zikionesha wagonjwa wa Ukoma kulia ni Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
...................................................................................................................................
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani kuazimisha siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa tarehe 29 Januari 2016 kwa kutoa elimu juu ya kujikinga na kupambana na Ukoma Tanzania na kuifanya Tanzania iweze kuondokana na m aambukizi mapya ya ukoma. Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ikiwa ni harakati za serikali kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa elimu kwa umma wa watanzania. Mhe.Ummy Mwalimu amesema siku hii itawapa fursa ya kutathimini mwelekeo wa jitihada za nchi na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu ambao umekuwa ukiogopwa sana katika jamii yetu toka enzi na enzi hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kuduma. “Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014,jumla ya wagonjwa 2,134 wa Ukoma waligunduliwa ambapo wagonjwa 271 kati ya hao ambao ni sawa na asilimia 13walikuwa na ulemavu na pia bado kuna Wilaya 17 za Tanzania bara na 2 za Tanzania Visiwani zilizogunduliwa idadi kubwa ya wagonjwa wa Ukoma” “ Nizitaje wilaya hizi ambazo zimekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Ukoma kwa Tanzania Bara ni Liwale,Ruangwa,Lindi Mjini,Lindi Vijini,Masasi Vijijini,Newala,Nanyumbu,Namtumbo,Tunduru,na Nkasi. Nyingine ni Mkinga,Muheza,Korogwe,Musoma,Korogwe,Musoma Vijijini ,Chato,Shinyanga Manispaa na Rufiji na kwa Tanzania Visiwani ni Mkoa wa Mjini Magharibi na katika wilaya za kati na kusini. Alisema Mhe Mwalimu. Aidha amesema kuwa Tanzania katika kuadhimisha siku hii Serikali inayashukuru mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa michango yao katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukoma hapa Tanzania na hivyo kuhakikisha tunakuwa na Tanzania isiyo na maambukizi mapya ya Ukoma. Tanzania ni miongoni mwa nchi 17 Duniani ambazo bado zina viwango vya juu vya ugonjwa wa Ukoma na kwa zaidi ya miaka 62, siku ya ukoma Duniani imekuwa ikiadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wa Januari.

Thursday, 28 January 2016

TFF YAPATA MSIBA MZITO...

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
TFF itawajulisha mipango ya msiba na mazishi ya marehemu Epaphra Swai baada ya kukaa na familia ya marehemu na kupanga utaraibu huo.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.


President of Tanzania Football Federation 
 

PresidentsTFF

 

 

CUF NA AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR



Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali. Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.

2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

3. KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.

4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.

5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.

6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke. Baraza Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.

8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar. Baraza Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.

9. KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.

10. KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.

11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani. Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.

12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.


LIMETOLEWA NA:

BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)

DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016

PICHA MBALIMBALI ZIKIMUONYESHA WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIBADLISHANA MAWAZO NA BAADHI YA WABUNGE NJE YA UKUMBI WA BUNGE MJINI DODOMA

majl1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Januari 28, 2016. Kutoka kushoto ni Jumanne Kishimba wa Kahama, Edwin Ngonyani wa Namtumbo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Hussein Amar wa Nyangwhale, Prosper Mbene wa Morogoro Kusini na Joseph Kalanda wa Sikonge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
majl2

Matukio Bungeni katika picha bungeni Dodoma leo

mh1
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh2
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akielezea juu ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ya kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro.
mh3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera,Uratibu na Bunge Mhe.Jenesta Mhagama akieleza juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali mara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro watu 30 wameokolewa katiaka ajali hiyo.
mh4
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali yahusuyo Wizara yake katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh6
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi(kushoto) na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi (kulia) wakifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
mh7
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh8
Mbunge wa Ilala (CCM) Mhe. Mussa Hassan Zungu akiuliza swali katika moja ya kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
mh9
Baadhi ya wabunge wakifatilia moja ya kikao katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
mh10
Wabunge wa upinzani wakitoka ndani ya Bunge mara baada ya kuanza kujadili hotuba ya Rais
picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

JULIAN BANZI ATEULIWA KUWA NAIBU GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA


Wednesday, 27 January 2016

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA ZA WABUNGE KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA LEO,


NDE2
Waziri Mkuu, Kassim Majalliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama Buneni mjini Dodoma Januari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NDE3
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa Elimu , Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce  Ndarichako, bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NDE4
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo  Nape Nnauye akitoa  kauli Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
NDE6
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016. Kutoka kushoto ni Ruth Mollel wa Viti Maalu Chadema, Hawa Mwinga wa Viti Maalum Cahdema na  Ali Saleh wa Malindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NDE7

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016. Kutoka kushoto ni Ruth Mollel wa Viti Maalu Chadema, Hawa Mwinga wa Viti Maalum Cahdema na  Ali Saleh wa Malindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NDE8

Mwenyekiti wa Bunge, Mtemi Andrew Chenge  akiongoza kikao cha Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NDE9
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Bungeni mjini Dodoma January 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA HAPA NCHINI, MAKAO MAKUU YA CCM, DAR ES SALAAM



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akimkaribisha Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Balozi akisaini kitabu cha wageni
Balozi akisaini kitabu wa wageni
Mazungumzo yakiendelea
Balozi huyo akimsalimia Ofisa wa Chama katika Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Gift Msuya
Balozi huyo akimsalimia Ofisa wa Chama katika Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Salehe Mhando
Wakijiweka sawa kwaajili ya kuendelea na mazungumzo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube