BREAKING

Wednesday 27 January 2016

BONNY MWAITEGE :TAMASHA LA PASAKA TULIPE UZITO WAKE


bo1
 
Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injil, Bonny Mwaitege ametoa wito kwa Watanzania kuilipa uzito wa aina yake Tamasha la Pasaka kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tukio hilo adhimu duniani.
Mwaitege alisema Tamasha la Pasaka lina ujumbe wa Mungu hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi na kumkimbilia M
ungu katika tamasha hilo.
“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, hivyo kuna kuna ujumbe mkubwa  kutoka kwa Mungu ambao utawaokoa Watanzania wote,” alisema Mwaitege. 
Mwaitege alisema kupitia tamasha hilo jamii inaondokana na machafu ambayo yanamchukiza Mungu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufanikisha matakwa ya jamii kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na viongozi wa dini watakaohudhuria tamasha hilo.
Msama alisema tamasha la mwaka huu wamepanga litaanza Machi 26 hadi 28 hapa nchini, hivyo Watanzania wajiandae na tamasha hilo.
“Watanzania watarajie tamasha bora ambalo litafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii, hivyo wajiandae,” alisema Msama.
------------------------------------------------------

PINDA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UTAMADUNI WA WACHINA.

pin1
Mwambata wa Utamaduni katika Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China Bw. Gao Wei akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano kuelezea maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zitazofanyika Januari 30 mwaka huu jijini Dar es salaam.
pin2
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Mwambata wa Utamaduni katika Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. Gao Wei hayupo pichani wakati wa mkutano kuelezea maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zitazofanyika Januari 30 mwaka huu jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY  DAUD -MAELEZO

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube