BREAKING

Thursday, 7 January 2016

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA IKULU, JAJI WARIOBA NAYE YUMO, WATETA JUU YA UFISADI NCHINI......



Rais Dk.John Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU imesema kuwa Mara baada ya mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi na kuunda Serikali pamoja an kumtakia heri ya mwaka mpya 2016.


Rais Mstaafu Mkapa amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya mwaka mpya , amempongeza Rais Magufuli  kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi ya serikali apamoja na kuelekeza fedha kwenye maeneo muhimu ambayo yanagusa wananchi, huku akiwaomba wananchi  kumuunga mkono Rais Magufuli katika kukomesha rushwa na ufisadi.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube