Zoezi la kuweka Alama za X kwenye nyumba zinazopaswa kubomolewa limeendelea leo katika maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam ambapo nyumba zaidi ya 3500 zimewekwa alama hiyo katika eneo la bonde la mto Msimbazi.
**Katika kutekeleza zoezi hilo, zaidi ya askari elfu moja wa kikosi cha kuzuia ghasia FFU cha Jeshi la Polisi wameimarisha Ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mabondeni kutokana na kushambuliwa kwa mawe hivi karibuni baadhi ya maafisa kutoka ardhi waliokuwa wakiendesha zoezi hilo katika maeneo ya jangwani ambapo wananchi pia walifunga barabara kwa matairi na kuchoma moto kupinga zoezi hilo.
Maeneo yaliyokumbwa na zoezi la kuwekwa alama za x ni pamoja na nyumba zote zilizopo eneo la jangwani, upande wa kigogo sambusa,kigogo mbuyuni pamoja na nyumba zilizopo katika eneo la sukita , ambapo utekelezaji wa kuweka alama hizo umewaacha baadhi ya wamiliki wakiangua vilio ,wengine kuanguka na kupoteza fahamu huku baadhi wakiduwaa kwa kushindwa kujua hatua gani wachukue kutokana na wengine kuwa na majengo mapya ya gharama ambayo wamejenga kando ya mto msimbazi.
Akizungumza na mtandao huu wa Shamakala360 Afisa mwandamizi kutoa baraza la taifa la usimamizi wa mazingira NEMC- Anold Kisiraga amesema zoezi la kubomoa nyumba linaanza rasmi kesho kwa wale waliopinga kubomoa kwa hiari yao huku pia akisisitiza kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na uwekwaji wa alama za x kwenye nyumba ambazo zitakumbwa na zoezi hilo.
Wakati huo huo Ombi la wakazi zaidi ya 600 wa mabondeni wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni ambao wamefungua kesi katika mahakama ya kuu kitengo cha ardhi kusitishwa zoezi hilo limesogezwa mbele mpaka kesho saa tano .
No comments:
Post a Comment