Wednesday, 31 January 2024
WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA MATAIFA 8 KUSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA 2024
Thursday, 25 January 2024
TAMASHA LA PASAKA 2024 KUANZIA JIJINI DAR ES SALAAM,MACHI 31
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Alex Msama ametangaza Tamasha la Pasaka mwaka 2024 linatarajia kuanza kufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam siku ya Pasaka tarehe 31 mwezi 3 mwaka 2024
Waimbaji mbali mbali wa muziki wa Injili watashiriki katika Tamasha hili kubwa la Pasaka kwa mwaka 2024.
Maandalizi makubwa yanaendelea kufanyika, na Tamasha la mwaka huu limekuja na kauli mbiu inayosema "
ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MCHAPA KAZI.....
Monday, 22 January 2024
SPORTPESA WAIUNGA MKONO TAIFA STARS AFCON KWA PROMOSHEN
Afisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Lydia Solomon, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya Sportpesa AFCON
RAIS SAMIA :JESHI LA WANANCHI JWTZ JIPANGENI UCHAGUZI UNAKUJA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) Dkt. Anna Makakala kwenye picha ya pamoja na Maafisa Wanawake wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kufungua Mkutano wa CDF na Makamanda kwa mwaka 2023 uliofanyika Lugalo Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari, 2024.
Monday, 15 January 2024
KATIBU MKUU MPYA CCM USO KWA USO NA RAIS SAMIA
EMMANUEL NCHIMBI KATIBU MKUU CCM..
KAMISHNA MABULA AFANYA UKAGUZI WA KARAKANA YA KISASA MANYONI, ATOA MAELEKEZO MAHSUSI
Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda ameeleza kufurahishwa kwake na ubora wa viwango vya ujenzi wa karakana ya matengenezo ya magari na mitambo iliyojengwa Kanda ya Kati ya TAWA wilayani Manyoni, karakana inayotajwa kuwa ni kubwa kuliko karakana zote zilizojengwa na taasisi hiyo.
Ameyasema hayo Januari 14, 2024 akiwa katika ziara yake Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya TAWA wilayani Manyoni, ziara yenye lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na utalii zinazotekelezwa na TAWA wilayani humo.
"Nimetembelea na kukagua karakana, kimsingi nimeona imejengwa vizuri na pia nimeona ina uwekezaji mkubwa wa vifaa vitavyotumika na nina imani hii karakana itatusaidia sana" amesema
Akibainisha sababu za kuifanya karakana hiyo kuwa kubwa wilayani humo, Kamishna Mabula amesema Manyoni ni katikati ya nchi na ni sehemu inayofikika kwa urahisi, hivyo kutokana na ukubwa wake itatumika kutengeneza magari si tu ya Kanda ya Kati bali ya taasisi nzima.
Aidha, Kamishna Mabula ameuelekeza uongozi wa Kanda hiyo kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa karakana ikiwa ni pamoja na kuwapeleka wataalamu wa vifaa hivyo ili iweze kusimamiwa na kuendeshwa Kisasa.
Vilevile Kamishna Mabula ametumia ziara hiyo kuwahimiza Maafisa na Askari wote wa TAWA kurejea mpango mkakati wa taasisi hiyo ambao unafikia kikomo Mwaka 2026 ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Amefafanua kuwa mpango mkakati wa TAWA una malengo makuu matatu ambayo ni kuhakikisha rasilimali ambayo TAWA imepewa kusimamia inakuwa salama, pia kuhakikisha wateja wote wa taasisi wakiwemo wawekezaji wanapata huduma na kuridhika na huduma inayotolewa na lengo la tatu ni kuhakikisha TAWA inafanya kazi kwa ufanisi na tija.
Kamishna huyo amesisitiza kuwa malengo hayo hayataweza kutimia bila kuishi katika tunu za taasisi hiyo ambazo ni uadilifu, kufanya kazi kwa ushirikiano, kutenda kazi kwa ubunifu pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
Naye Kamishna Msaidizi Ulinzi wa Rasilimali za Wanyamapori Hadija Malongo akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa Kanda ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TAWA kwa kuwezesha ujenzi wa karakana hiyo ambayo kukamilika kwake kutasaidia kupunguza gharama za matengenezo ya magari ambayo ilikuwa changamoto kubwa
Mradi wa ujenzi wa karakana hiyo umegharimu zaidi ya TZS Million 217.
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Leo tarehe Januari 15, 2023 Unguja, Zanzibar
Thursday, 11 January 2024
MKAZI WA KAGERA OLIVIA PASTORI AKABIDHIWA MIL. 10 ZA MAJIFTI DABODABO KUTOKA TIGO
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Shilingi milioni kumi Mshindi wa Magifti Dabodabo mkazi wa kijiji cha Rushaka, Kitongoji cha Bweigilo kata ya Bwendangabo wilayani Bukoba mkoani Kagera Olivia Pastory baada ya kuibuka mshindi katika hafla iliyofanyika nyumbani kwao mshindi,katikati ni Meneja wa Tigo Mkoa wa Kagera Robert Paul akishuhudia.
Tuesday, 9 January 2024
MLOGANZILA WAZINDUA HUDUMA YA MAFUNZO YA WAGONJWA WA KIHARUSI
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Taasisi ya Kiharusi Duniani (The World Stroke Organization) imezindua mafunzo maalumu kwa wataalamu wanaoshughulikia magonjwa ya kiharusi kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma kwa wagonjwa hao.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya nje (OPD) Dkt. Elimeena Meda amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kiharusi hivyo ni muhimu watoa huduma wote kujua namna bora ya kuwahudumia wagonjwa hao.
“Tumeona sababu ya kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa kiharusi, mafanzo haya yanahusu kada zote zinazoshiriki katika mnyororo wa kuwahudumia wagonjwa wa kiharusi ili kuboresha huduma wanapokuwa hospitalini hadi wanaporuhusiwa” ameongeza Dkt. Meda.
Kwa upande wake, muandaaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt. Sarah Matuja amebainisha kwamba ugonjwa wa kiharusi umekuwa tishio nchini na unawakumba watu wenye umri wa miaka kati ya miaka 40 hadi 60 na hivyo kuathiri nguvu kazi ya jamii.
Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu bingwa wa magonjwa ya kiharusi duniani kuanzia leo Januari 9 hadi Machi 19, 2024 ambapo yatahusisha wakufunzi ambao ni Madaktari Bingwa wa kiharusi duniani na yatafanyika kwa nadharia na vitendo.
TIGO WADHAMINI WA MAONYESHO YA KIBIASHARA ZANZIBAR
Mkurugenzi wa kanda Tigo Zantel, Aziz Said Ali, akimuelezea Mshafanyabiashara wa Mwani, Jaha Haji Khamis kuhusu huduma ya Mjasiriamali box katika maonesho ya kibiashara Zanzibar,ambapo Tigo zantel ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Saturday, 6 January 2024
DKT. BITEKO- TUYAENZI NA KUYALINDA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuyaenzi, kuyalinda na kuyaishi kwa dhamira ya dhati, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwani Waasisi wa Nchi walifanya mapinduzi hayo ili kuwa na Taifa huru ambalo kila mtu anakuwa na hadhi, kuondoa dhuluma iliyokuwepo na kufanya wananchi kuishi kwa amani na furaha.
Amesema hayo tarehe 6 Januari 2024 wakati akizungumza na Wananchi katika Wilaya ya Mkoani, mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua Afisi ya Uhamiaji na Makaazi ya Askari wilayani humo.
“Sisi Wananchi tunawajibu wa kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuyaishi, kuyaheshimu, kukuza uchumi wa nchi na kukuza uzalendo ili baada ya muda mrefu hata baada ya miaka 100 mbele, watakaokuja kusherehekea Mapinduzi haya wakute Zanzibar iliyobora zaidi na waseme Mapinduzi haya yalitufaa.” Amesema Dkt. Biteko
Ameeleza kuwa, moja ya tunu tuliyonayo ni mshikamano hivyo watu wasiruhusu mtu yoyote kuwagawanya kwa misingi yoyote ile, bali maendeleo yaunganishe watu wote na kwamba tofauti za vyama, dini na kabila visifanye watu wakae kwenye makundi bali kuunganisha watu kwa maslahi ya nchi na watanzania.
Amesema kuwa, nchi inapoenda kusherehekea Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari mwaka huu, watanzania wote waungane kuwaombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, ili waendelee kuongoza vyema, kuimarisha ustawi wa Taifa na kuwaunganisha Watanzania.
Kuhusu Jengo hilo jipya la Afisi ya Uhamiaji katika Wilaya ya Mkoani, mkoani Kusini Pemba, Dkt, Biteko amesema kuwa ni moja ya matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani kabla ya Mapinduzi watu walinyimwa haki zao za kimsingi zikiwemo za uhamiaji kama vile kupata pasi ya kusafiria na hivyo Mapinduzi yamewezesha wananchi kupata uhuru wa kusafiri nje ya mipaka ya nchi.
Friday, 5 January 2024
MAGIFTI DABODABO YA TIGO -MUUZA MATUNDA ALAMBA MIL.5...
Kampeni ya Magifti Dabodabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, imewakabidhi mamilioni yao washindi wa kampeni hiyo waliopatikana wikiendi iliyopita.
Katika tukio hilo washindi watatu, Flazia Issa, Stephano Mgova, Shabani Juma walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja na Kiungi Juma alikabidhiwa shilingi milioni tano alizojishindia.
Akiwakabidhi mfano wa hundi ya fedha walizojishindia Semaji la Kampeni hiyo, Haji Manara aliwapongeza washindi hao na kuwataka wakawe mabalozi wazuri wa kampeni kwani wao ndiyo mashuhuda wakubwa wa ukweli na uwazi wa kampeni hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa za Tigo, Ndevorael Eliakimu aliwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo kwa huduma mbalimbali kama vile kufanya miamala, kulipa bili na malipo mengine, kununua vocha kwa kutumia Tigo Pesa au za kukwangua na huduma nyinginezo.
Eliakimu amesema kampeni bado inaendelea ambapo pamoja na pesa taslimu kuna zawadi za seti ya vifaa vya nyumbani vya kisasa kutoka Kampuni ya Hisense ikiwemo friji, runinga, microwave na seti ya muziki (sound bar).
Sambamba na zawadi hizo, Eliakimu amesema kuna zawadi kubwa za magari mapya kabisa ya kisasa ambapo zawadi zote hizo zitatolewa mara mbili kwa kila mshindi na mpendwa wake kama inavyoitwa kampeni hiyo Magifti Dabo dabo.
Wednesday, 3 January 2024
SERIKALI YANUFAIKA NA ZAIDI YA BILIONI 600.…
Serikali imesaini mikataba mitano ya uwekezaji Mahiri kwa wawekezaji wa wanyama pori nchini ambapo Serikali itanufaika na zaidi ya shilingi bilioni mia sita tisini za kitanzania ikiwa na lengo la kuvutia na kuendeleza vivutio vilivyopo nchini vinavyomilikiwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA) ikiwa ni jitihada za rais wa awamu ya sita Mh Rais Dkt Samia Suluu Hassan katika kukuza utalii wa ndani na kuwanufaisha watanzania wote.....
Waziri wa maliasili na utalii Angela Kairuki amesema hii ni nafasi kwa serikali ya Tanzania kupitia Mhe Rais samia kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji na kuendelea kuwavutia wawezekaji na kuongeza idadi ya wawekezaji nchini
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi ya (TAWA) Hamis Semfuko amesema lazima kuboresha miundombinu ambayo inamilikiwa na tawa ili kuvutia utalii wa ndani katika maeneo mbali mbali…
Mmoja kati ya wawekezaji katika hafla hiyo Taral Abood amesema kupitia uwekezaji huo wanaenda kutekeleza na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita katika kupiga hatua za kimaendeleo…
Hafla hiyo ya utiaji wa saini ya mikataba sita umehudhuriwa na wakala wa misitu tanzania tfs, mamlaka ya usimamizi wa nyamapori tanzania tawa, na wawekezaji pamoja na wadau kutoka sehemu mbali mbali.
Tuesday, 2 January 2024
KINANA AWASILI RUANGWA, AHUTUBIA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYANI HUMO.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewasili wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikakazi ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Chama wa wilaya hiyo.
Kinana amewasili wilayani humo leo Januari 1, 2024 akiambatana na viongozi mbalimbali wa Chama wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Akiwa wilayani humo kesho atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa ambao pia utahudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa.