BREAKING

Thursday 30 August 2018

MULTCHOICE TANZANIA YATANGAZA WASHINDI WATAKAOPATA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU NAIROBI....



image.png
  
MultiChoice Tanzania, Imetangaza  washindi  wanne waliokidhi vigezo katika shindano la MultiChoice Talent Factory lilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka huu . Programu hii itawezesha jumla ya vijana 60 kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika kuweza kupata mafunzo ya filamu kwa kipindi cha mwaka mmoja katika vituo vitatu tofauti, kimojawapo kikiwa nchini Kenya (Nairobi) ambapo vijana hawa watakuwapo ifikapo tarehe 01 Oktoba mwaka huu.

Mchakato mzima  wa kupatakana kwa washindi hawa ulichukua takribani muda wa miezi miwili ambapo kwa hapa nyumbani Tanzania tulipokea maombi kutoka kwa vijana zaidi ya 160, yaliyofuatiwa na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai Mwaka huu hapa Dar es Salaam Tanzania.Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, ndugu Alpha Mria akielezea kwa undani namna mchakato huu wa kupata vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye sekta ya Filamu na mwisho kupatikana washindi hawa wane ambao mnamo Octoba 2018 wataenda kuiwakilisha Tanzania kwenye ya Mafunzo Maalum ya Tasnia ya Filamu MultiChoice Talent Fatory,  huko Jijini Nairobi Kenya kwa kipindi cha mwaka mzima.

“Maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi tulizonazo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, na kadhalika huku sekta ya ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo sekta ya sanaa na ubunifu kuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa uchumi wetu. Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha program hii na tumeanza na sekta ya filamu. Vijana wa kitanzania waliofanikiwa kufudhu katika mchakato huu ni Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, Wilson  Nkya kutoka Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, alisema Alpha Mria  Meneja Masoko MultiChoice Tanzania.

image.png

Picha ya Pamoja ya Uongozi wa Multichoice Tanzania wakiwa na Vijana walioibuka kidededea watakao kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mafunzo Maalum ya Filamu Multichoice Talet Factory, jijini Nairobi Kenya, kutoka kusho ni Jamal Kishuri kutokea Arusha, Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, katikati ni Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifuatiwa na mshindi Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, pembeni ni Menejea Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria na mwisho kulia ni mshindi wetu mwingine Wilson  Nkya kutoka Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo.

Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu bila shaka tutafanikiwa kupanua wigo wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Amesema mafunzo hayo yataanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu itawawezesha vijana hawa wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filamu ambavyo vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia. Kwa upande wao, washindi waliotangazwa kufudhu katika program hii wametoa shukrani zao za dhati hususani kwa kampuni ya MultiChoice sambamba na serikali ya Tanzania kwa ujumla. Akiongea katika hafla nhiyo, Wilson Nkya mmoja kati ya vijana waliopata fursa hiyo alisema kuwa “ Kipekee hii ni fursa tuliyokuwa tukiisubiri kwa muda mrefu na tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Kampuni ya MultiChoice, serikali na jamii yote kwa ujumla.  Tunaahidi kufanya kila liwezekanalo na mtegemee matokeo chanya kutoka kwetu’, alimalizia Wilson.
image.png
Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria wakiwapongeza vijana hawa wakitanzania walioibuka washindi wa mpango huu wa kukuza tasnia ya Filamu Afrika unaotambulika kama Multichoice Talent Factory, vijana hawa wataliwakilisha Taifa kwenye mauzo haya maalum ya mwaka mzima yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya, kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakiwa yameandaliwa na kugharamiwa na MultiChoice Afrika.

Wednesday 29 August 2018

RWANDA-YANGA KUSHUKA DIMBANI LEO KUIVAA RAYON SPORTS


Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba na Rayon huku ikiwa haina nafasi yoyote ya kusonga mbele.

Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema wachezaji wote wako vizuri kiafya na hakuna yoyote ambaye yuko majeruhi.

Saleh ameeleza lengo lao kubwa kwenye kipute hicho ni kuweka heshima ya kuhakikisha wanapata matokeo licha ya kuwa hawana nafasi ya kusonga mbele.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki ambapo itachezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo uliopo jijini Kigali.

Yanga ilianza michuano hiyo kwa kusua sua baada ya kukubali vipigo vikubwa viwili, wakati ilipokutana na USM Alger ya Algeria nchini Algeria na kuchapwa mabao 4-0 na Gor Mahia kuwachapa idadi kama hiyo.


Timu hiyo ilijitutumua ilipocheza Dar es Salaam, na USM Alger baada ya kuifunga timu hiyo mabao 2-1

DROO YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA KUPANGWA LEO SAA MOJA





  • Klabu nne za England watatambua wapinzani wao katika awamu ya makundi ya mashindano ya kuwania ligi ya mabingwa Ulaya wakati droo itakapofanyika leo Alhamisi.

  • Manchester City itakuwa katika chungu cha kwanza na Manchester United na Tottenham Hotspur katika chungu cha pili huku Liverpool ikiwekwa kwenye chungu cha pili au cha tatu.
Droo inatarajiwa kufanyika Grimaldi Forum huko Monaco mwendo wa saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.

Mabingwa kombe hilo ni Real Madrid ambao waliwafunga Liverpool katika fainali


MTOTO WA JINSIA MBILI YA KIKE NA KIUME AZALIWA MULEBA MKOANI KAGERA



Mtoto wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Geore Kasibante (pichani),  ambaye alisema hali ya mtoto huyo kuwa inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospila hiyo hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.

Monday 27 August 2018

DSTV YANGEZA CHANNEL MPYA YA KIHINDI........

Moto Hauzimi na DStv, Star Life nyumba ya Bollywood sasa ndani!

Kampuni ya Multichoice inajivunia kuongeza chaneli  mpya ya filamu inayojulikana kwa jina la Star Life mahususi kwa ajili ya wapenzi wa filamu  na Tamthilia za kihindi.

Chaneli hii yenye maudhui ya kihindi inayorusha matangazo kwa Lugha ya kingereza imeanza rasmi kupatikana tarehe 27 Agosti 2018 chaneli namba DStv 167 iliyopo kuanzia kifurushi cha DStv Family.

Wateja wa DStv na watanzania wote kwa ujumla wataweza kufurahia filamu nzuri na za Kisasa za kihindi, Tamthilia na Series kali zenye kugusa hisia na tamaduni na maisha ya kihindi na vipindi vingine mbalimbali vya burudani kupitia chaneli hii vitakavyokuwa rushwa hewani kwa lugha ya kiingereza.

Kwa zaidi ya miaka 20 chaneli hii imekuwa ikipeperusha bendera kwa kuwa chaneli namba  moja kutokana na ubora wa maudhui ya filamu na sinema zilizosheni  ndani yake.

“Nyongeza ya chaneli hii ni matokeo ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma za DStv kwa burudani za kisasa kabisa ambazo hawatoweza kuzipata kwingine kokote. Chaneli hii itakuwa ikipatikana ndani ya DStv kupitia chaneli namba 167 kuanzia kifurushi cha Family 39,000.

Hakika Moto Hauzimi na DStv!


Thursday 16 August 2018

MULTICHOICE TANZANIA YAWAZESHA VIJANA YAWAFUNGULIA OFISI MAWAKALA WAKE MAMBO NI MOTOOOOOO!


Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeimarisha mkakati wake wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Katika kutimiza hilo kampuni hiyo imekabidhi ofisi na bajaji tisa kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na inatarajia kupanua mradi huo kwenda mikoa mingine ikiwemo Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.

Akizungumza katika makabidhiano ya Bajaji hizo yaliyofanyika leo Alhamisi Agosti 16 katika makao makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum, amesema hii ni awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo wametoa jumla ya bajaji 27 kwa viunga 9 vya Dar es salaam na kwamba baada ya awamu hii watafanya tathmini na kisha kuupanua hapa Dar es Salaam ni mikoa mingine.

Amesema katika mradi huo, MultiChoice inawafadhili vijana hao ofisi za uwakala wa DStv na pia inawadhamini vitendea kazi muhimu kama vile Kompyuta na Bajaji ili viwawezeshe kufanya kazi zao kwa ufanisi.

2

Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mmoja wa mawakala wapya wa mauzo wa DStv wa kiunga cha Temeke Rose Haule wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

“Tumekuwa tukifanya kazi na vijana wengi ambao ni mawakala wa mauzo wa kujitegemea (direct sales) lakini sasa tumeamua tuwafanye wabia wetu wa kibiashara na kuwawezesha kuendesha biashara rasmi ya uwakala wa DStv” alisema Salum na kuongeza kuwa vijana hao watakuwa wakitoa huduma katika maeneo maalum yajulikanayo kama ‘viunga’. Kila wakala atakuwa na kiunga chake, na atakuwa na jukumu la kuhakikisha wateja wa eneo lake wanahudumiwa kwa haraka

“Vijana hawa watakuwa na mtandao wa vijana wengine wa mauzo na mafundi wa kufunga DStv ambao wamepata mafunzo maalum na kuthibitishwa. Kwa hiyo, kama mteja yuko Mbagala, atahudumiwa na wakala wa kiunga cha Mbagala, hivyo hivyo aliyeko Tabata atahudumiwa na kiunga cha Tabata na hii itakuwa kwa viunga vyote ambavyo ni Mbagala, Tabata, Kigamboni, Ilala, Chang’ombe, Mbezi beach, Mbezi Kimara, Manzese na Ukonga.

3
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum (wa pili Kulia) akizungumza na kiongozi wa Kiunga cha DStv Temeke Rose Haule (wa pili Kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj). Kulia ni Khalfani Soni na kushoto ni Omari Ali wote wa Gongo la Mboto.

Amesema kwa kuwarasimisha vijana hawa, sasa watakuwa wanafanya biashara rasmi, wakiwa na leseni na ofisi na hivyo kuweza pia kulipa kodi stahiki kwa serikali na hivyo kuongeza mchango wao kwa uchumi wa nchi.

Wakizungumza bara baada ya kukabidhiwa bajaji hizo sambamba na laptop, wakuu wa viunga hivyo wamesema wamekuwa wakifanya kazi kama mawakala wadogo wa kujitegemea kwa muda sasa lakini walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na ofisi rasmi na pia vitendea kazi hususan usafiri.

“Tulikuwa tunafanya mauzo kwa tabu sana kwani kwanza kutokuwa na ofisi ilikuwa ni vigumu kwa wateja kutupata. Pia hata ukipata mteja unalazimika kubeka vifaa kwenye usafiri usio wa uhakika kwenda kwa mteja na hii ilikuwa inapoteza muda na kuongeza gharama” alisema Rose Haule mkuu wa kiunga cha Temeke.

5
Wakala wa mauzo wa DStv Rose Haule wa Temeke (aliyeko ndani ya Bajaji) akifurahia na wenzake Khalfani Soni wa Gongo la Mboto,  Omari Ali wa Gongo la Mboto  na Sarah Makasia wa Manzese wakifurahia muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Naye Yusuph Migeto wa kiunga cha Mbagala amesema kuwa kuwepo kwa ofisi na usafiri wa uhakika kutawahakikishia wateja wao huduma ya haraka na yenye ufanisi. “wakati mwingine wateja walikuwa wanalalamika kwa kucheleweshewa huduma kwani ukipata mteja inabidi ufuate vifaa DStv kisha uende kumfungia mteja. Hii ilikuwa inachelewesha sana. Lakini kwa sasa tutakuwa na uwezo wa kuwa na vifaa karibu na pia kuwepo kwa usafiri wa uhakika kutatufanya kufanya kazi kwa haraka zaidi

NI ATLETICO MADIRD WASHINDI SUPER CUP YA UEFA...


















Timu ya Atletico Madrid imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kuwania taji la Super Cup ya Ulaya usiku wa jansa huu Uwanja wa A. Le Coq Arena mjini Tallinn, Estonia.

Shujaa wa Atletico Madrid  amekuwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Diego Costa aliyeipasua ngome ya Real Madrid mara mbili. 

Costa alifunga bao la kwanza mapema tu dakika ya kwanza akimalizia pasi ya Diego Godin, lakini mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema akaisawazishia Real dakika ya 27 akimalizia pasi ya Gareth Bale.

Nahodha, Sergio Ramos akaifungia bao la pili Real Madrid kwa penalti dakika ya 63, baada ya Juanfran kuushika mpira kwenye boksi.

Coasta akarejesha matumaini kwa Atletico baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 79 akimalizia pasi ya Muargentina, Angel Martin Correa na dakika 90 zikalazimika timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.

Saul Niguez Esclapez akaifungia Atletico Madrid bao la tatu dakika ya 98 akimalizia pasi ya kiungo Mghana, Thomas Teye Partey na Jorge Resurreccion Merodio, maarufu kama Koke akaifungia bao la nne timu hiyo dakika ya 104 akimalizia pasi ya Víctor Machin Perez au Vitolo kwa jina maarufu zaidi.

Wednesday 15 August 2018

KIKOSI CHA KINACHOWAVAA ARUSHA UNITED JIONI HII

Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Arusha United leo

1. Aishi Manula 
2. Nicholas Gyan
3. Asante Kwasi 
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa 
6. Jonas Mkude 
7. Shiza Kichuya 
8. James Kotei
9. Meddie Kagere
10. Emmanuel Okwi 
11. Hassan Dilunga

TFF YAJITOKEZA YASEMA MSIMU WA LIGI MPAKA SASA WANA WADHAMINI WAWILI....


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi limeweka wazi kuwa ligi kuu msimu ujao itakuwa na wadhamini wawili ambao ni Azam Pay TV na Benki ya KCB baada ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kumaliza mkataba wake.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, inasema kuwa ligi hiyo itakuwa na wadhanini hao ambapo Azam watakuwa na haki ya matangazo wakati KCB wakiwa ni wadhamini wenza kwenye ligi hiyo.

Barua hiyo imeeleza kuwa udhamini huo utakuwa na malipo ya kiasi cha sh milioni 162 kutoka Azam Pay TV kwa klabu, wakati malipo kutoka KCB yakiwa ni sh milioni 15.

Kufuatia barua hiyo kutoka Bodi ya Ligi Championi Jumatano lilimtafuta rais wa TFF, Wallace Karia ambaye alifunguka kuwa: “Suala la wadhamini litakapokuwa tayari litawekwa wazi kwa sababu tuna utaratibu wa kuwajulisha wadau wetu maana mtachokonoa matokeo yake tukatoa taarifa ambazo zinatuharibia mipango yetu,” alisema Karia.

Kutoka Championi.

Tuesday 14 August 2018

UEFA SUPER CUP MAMBO NI MOTOO!!!

UEFA SUPER CUP Jumatano hii kule Hispania mambo ni hivi, mambo ni moto!!

Nani atakuwa bingwa ya Super Cup, kati ya Real Madrid Na Atletico Madrid Jumatano hii? Usikose mechi hii kali ya mabingwa hawa mawili wakiwania ubingwa wa jumla wa Super Cup ndani ya DStv , Ni  Jumatano hii saa 4 usiku kupitia Supersport 3 iliyopo kwenye DStv pekee kifurushi Compact kwa sh.69,000 tu!

Bila kusahau, wateja wa DStv wanaweza pakua “Download Application”  ya DstvNow  itakayowawezesha watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida ukiwa mahali popote wakati wowote bila gharama ya ziada!


Ukiwa Na DStv, soka ni mwanzo mwisho yani Moto hauzimi, na kama sio DStv, Potezea!

Monday 13 August 2018

BODI YA LIGI NI MWENDO WA MABADILIKO....

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube