Dar
es Salaam Jumatano November 15, 2017; Kama ilivyo ada, katika msimu huu
wa sikukuu, Multichoice tanzania imetangaza neema kwa watanzania kwa
kutoa ofa
kabambe kwa wateja wake ambapo kuanzia leo mteja mpya wa DStv ataweza
kuunganisha kwa shilingi 79,000 tu hii kikiwa ni vifaa vyote pamoja na
kifurushi cha DStv Bomba cha mwezi mzima.
Akizungumzia
ofa hiyo, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Hilda
Nakajumo, amesema kuwa Multichoice imekuwa na utamaduni wa miaka nenda
rudi
wa kuwapa zawadi wateja na watanzania kwa ujumla na kwamba kila ufikapo
msimu kama huu DStv huwatunuku wateja wake ili kuwawezesha kufurahia
zaidi msimu huu wa sikukuu.
Tunafahamu
kuwa msimu huu wa sikukuu familia nyingi zinaungana katika
kusherehekea, hivyo DStv imeamua kuwaongezea burudani kwa kutoa ofa hii
kabambe. Amesema
badala ya mteja mpya kulipa shilingi 98,000 kwa ajili ya kuunganishwa
pamoja na kifurushi cha mwezi, sasa watalipa shilingi 79,000 tu na
kuunganishwa na DStv pamoja na kifurushi cha Bomba cha mwezi mzima.
“Tunapokuwa
nyumbani na familia zetu, watoto wanataka waangalie katuni, sisi
kinamama tunapenda kuangalia vipindi kama vile vya mapishi, urembo, na
tamthilia,
kinababa nao hupenda sana kutazama michezo mbalimbali kama kandanda na
kadhalika. Ni kwa msingi huu tumeamua kuwarahisishia burunani hii
inayopatikana kutoka DStv” alisema Hilda na kuongeza kuwa wataendelea
kutoa ofa kwa wateja wao kila inapihitajika.
Ofa hii ni kwa nchi nzima na itaendelea kwa miezi miwili hadi Januari 15, 2018
Ofa
hii kwa wateja wapya inakuja siku chache tu baada ya DStv kuanza kutoa
zawadi kwa wateja wake kwa kuwaongezea chaneli za SuperSport kwenye
vifurushi vyao
punde walipiapo akaunti zao kabla hazijakatika.
Katika
ofa hii ya kuongezewa chanel, wateja wa kifurushi cha Compact na
Compact Plus watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika
kifurushi cha
DStv Premium kwa kipindi cha siku saba (7) mfululizo bureeee!
Hali
kadhalika, watumiaji wa kifurushi DStv Bomba na DStv Family nao
watapata chanel zote za Supersport zinazopatikana kwenye Kifurushi DStv
Compact na
hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (PL) na
mashindano mengine makubwa kwa siku saba (7) mfululizo bureee!
No comments:
Post a Comment