Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TANESCO |
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
TATHMINI
iliyofanywa na Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kufuatia
mfumo wa kupokea gesi asili kwenye mitambo ya kufua umeme, Kinyerezi I jijini
Dar es Salaam kupata hitilafu, imebaini matengeenzo makubwa yanahitajika
kufanyika ili kuhakikisha mfumo unarudi katika ubora wake..
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito
Mwinuka, iliyosambazwa kwa vyombo vya habari leo Novemba 1, 2017, imesema kufuatia
mfumo huo kupatwa na hitilafu majira ya mchana Oktoba 32, 2017, hatua ya kwanza
iliyochukuliwa na wataalamu wa TANESCO ni kuzima mitambo ili kuruhusu kazi ya
usafishaji kuondoa gesi hiyo kufanyika.
”Baada
ya usafishaji wa Mitambo kukamilika, matengenezo yalianza usiku wa kuamkia leo
Novemba 1, 2017, kwa kutumia wataalamu wa ndani wa Shirika pamoja na Mkandarasi
wa kampuni ya JACOBSEN ELEKTRO AS.” Taarifa hiyo ya TANESCO ilisema.
Taarifa
hiyo iliendelea kusema, “Kutokana na ukubwa wa matengeenzo na uangalifu wa hali
ya juu unaotakiwa katika kazi hii hususan suala la usalama wa mitambo pamoja na
watumishi wa Shirika waliopo katika eneo la mitambo, hatua za tahadhari
zimechukuliwa.” Taarifa hiyo ilisema.
Aidha
taarifa imefafanua kuwa kutokana na Mitambo hiyo kuzimwa ili kuruhusu kazi ya
marekebusho ya hitilafu hiyo kukamilika kwa wakati, kutakuwa na upungufu wa
umeme katika maeeno mbalimbali ya nchi.
“Uongozi wa Shirika
unawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa ujumla kwa maeneo ambayo bado
yanakosa huduma ya umeme katika kipindi hiki cha matengenezo hayo na
tutaendelea kuwaarifu wananchi jinsi kazi ya matengenezo inavyoendelea hadi
kukamilika kwake.” Taarifa hiyo ilisema
No comments:
Post a Comment