Timu ya Tanzania 'Taifa Stars' imeendelea kuwa mbabe wa timu ya Taifa ya Benin baada ya kuwaliazimisha wenyeji hao kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliokuwa katika kalenda ya FIFA.
Stars katika mchezo huo ilicheza kwa kujiamini huku ikiwa na kumbukumbu nzuri katika michezo ya nyuma dhidi ya taifa hilo kwa kuifunga mabao 4, lakini katika mchezo wa leo Stars walianza kufungwa kwa mkwaju wa penati iliyotolewa kiutata.
Hadi mapumziko Stars walikuwa nyuma kwa bao 1-0, kipindi cha pili Stars ilicheza kandanda la kuvutia wakigongeana pasi safi na hatimaye kufanikiwa kupata bao la kusawazisha likifungwa na mshambuliaji wake mahiri Elius Maguli, akipokea pasi murua kutoka kwa Shiza Ramadhan Kichuya.
Hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Stars walipata bao 1 na wenyeji bao 1
No comments:
Post a Comment