Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles
Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa
Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.
Kwa agizo hilo lililotolewa na
Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake
ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.
Simwanza anasimamishwa kazi kutokana
na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari
kutoridhisha.
Simwanza amehudumu katika nafasi
hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment