Wachezaji wa Yanga wakijifua katika Uwanja wa Uhuru |
wachezaji wa Yanga wakimsikiliza Kocha wao GeorgeLwandamina wakati wa mazoezi
Mabingwa wa Kandanda Tanzania Bara Yanga wameendelea na mazoezi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ikiwa ni matayarisho ya mchezo wao dhidi ya Singida United utakaopigwa katika dimba la Namfua mjini Singida.
Channel ten imeshuhudia wachezaji wa kikosi hicho wakijifua vilivyo chini ya kocha wao George Lwandamina huku baadhi ya wafanyakazi wa timu hiyo wakizuia waandishi wa habari kupiga picha mazoezi hayo.
Pamoja na changamoto hiyo Kamera ya Channel ten ilinasa baadhi ya matukio pamoja na mazoezi ambayo yaliuwa yakiendelea katika viwanja hivyo vya Uhuru Dar es Salaam.
Yanga wanaijiwinda na mchezo huo mgumu wa ugenini, dhidi ya timu ya Singida United ambayo imeleta mapinduzi makubwa tangu kupanda kwa daraja na kucheza Ligi Kuu.
Yanga itamenyana na singida ikitaka kupata pointi tatu ili kujitupa kileleni mwa Ligi kuu ambapo Simba ndio wanaongoza kwa sasa wakiwazidi wapinzani wao yanga kwa mabao ya kufunga, kwani kila timu ina pointi 16.
Mchezo huo pia utachangizwa kwa ushindani wa Singida United yenye alama 13 kutaka kuwakamata vinara wa Ligi simba kwa kushinda ili kufikisha pinti 16 na kuungana na vigogo wengine ambao ni Azam FC wenye pointi kama za Simba, Yanga pamoja na Azam FC
No comments:
Post a Comment