BREAKING

Friday 30 December 2016

KIUNGO 'MO' WA SIMBA LULU INAYOTEMBEA MBELE KWA MBELE, AIPA SIMBA POINTI TENA

Mohamed 'MO' Ibrahim akipongezwa na Kichuya

Mo akiachia shuti kali kwenye lango la Ruvu Shooting na kufunga bao pekee ,( Picha hii ni kwa Hisani ya Mtandao wa Bin Zubeiry)


Kiungo Mshambuliaji wa Simba Mohammed ‘Mo’ Ibrahim ameifungia bao pekee timu yake ya Simba katika ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Bao hilo alifunga katika dakika ya 45 kabla ya mapumziko na kuifanya sasa timu yake ya Simba kufikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi ya 18 na kuendelea kuogoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga.
  mdomo wazi kutokana na kuonyesha kiwango bora zaidi tangu alipotoka  Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Thursday 29 December 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA MWENYE UMRI WA MIAKA 82 CHATO MKOANI GEITA

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita
8
Mdogo wa Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na  kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.
Rais Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.
”Unapotokea msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi za uhai wa mzee”
Aidha Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare zake za shule wakati akisoma.
Kwa upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
29 Desemba, 2016

SPURS WAIFANYA ASUSA SOUTHAMPTON ST. MARY'S YAICHAPA MABAO 4-1

Tottenham walishinda mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Southampton usiku wa jana Uwanja wa St. Mary's kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya Spurs yalifungwa na Dele Alli mawili dakika za 19 na 87 na 85' Heung-Min Son dakika ya 85 wakati la wenyeji lilifungwa na Virgil van Dijk dakika ya pili tu ya mchezo

Wednesday 28 December 2016

DSTV YATOA ZAWADI YA SIKUKUU

DSTV
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya (kulia) akimkabidhi zawadi ya msimu wa Sikukuu ya Chris Mass na Mwaka Mpya kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale katika ofisi za mtandao huo Jijini Dar es Salaam. Zawadi hiyo kutoka kwa kampuni ya Multichoice Tanzania.
dstv-andrew
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya na Mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale wakiwa na zawadi hiyo wakati wa kukabidhi.
DSTV NA ANDREW CHALE
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya (kulia) akimkabidhi zawadi ya msimu wa Sikukuu ya Chris Mass na Mwaka Mpya kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale katika ofisi za mtandao huo Jijini Dar es Salaam. Zawadi hiyo kutoka kwa kampuni ya Multichoice Tanzania.

Kampuni ya Multichoice Tanzania wasambazaji wa visambuzi vya kisasa vya DSTV mapema leo 28 Desemba 2016, wametoa zawadi ya msimu wa Sikukuu kwa wadau wao mbalimbali ikiwemo kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao (Blog) wa MODEWJIBLOG, Ndugu Andrew Chale. Akikabidhi zawadi kwa niaba ya uongozi wa kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania, Costomer Retention Representative, Vida Msuya aliipongeza MO BLOG na mwanahabari huyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza vyema DSTV kwa muda wote na zawadi hiyo ni moja ya kurudisha fadhila kwa wadau wao. “Lengo la DST ni kuona tunazidi kuwa na wateja wengi ambao pia wanapata kitu bora kutoka kwetu. Huduma zetu nzuri na za kisasa hivyo kwa msimu huu wa Sikukuu wateja wetu na wadau tunawatembea na kuwapatia zawadi.” Alieleza Vida Msuya. Aidha, DSTV pia imeweza kuwapatia wadau mbalimbali zawadi hizo za Sikuukuu na kuwatakia kheri ya Mwaka mpya wa 2017. Aidha, kupitia kwa Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bw. Alpha Joseph hivi karibuni amebainisha kuwa katika msimu huu wa kusherehekea Sikukuu ya krismas na mwaka mpya wateja wao watapata kuangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza na zingine nyingi huku wakishusha bei za vifurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu kwa mwezi. 



WAZIRI MKU ANAVYOWATENDEA HAKI WANACHI VIJIJINI KWA KUZUNGUMZA NAO KATIKA ZIARA ZAKE HUKO RUANGWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Namilema wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi, Desemba28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Attachments area

YANGA WAITANDIKA NDANDA FC MABAO 4-0

 Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga imeendelea kuwafukuza kwa karibu wapinzania wao wa soka Simba baada ya hii leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Uhuru Dar es SAlaam

Yanga walianza kuliona lango la Ndanda mapema tu dakika ya nne likifungwa na mshambuliaji wao Donald Ngoma kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona.

Ndanda wakiwa katika hali ya kuwa na matumaini ya kurejesha bao hilo Yanga walifanikiwa kuongeza bao la pili katika dakika ya 21 likifungwa na Ngoma kwa mara nyingine akiuunganisha krosi safi ya Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na hatimaye kumfikia Ngoma aliyefunga kirahisi.

Ndanda ikiwa bado inajipanga Mshambuliaji Amis Tambwe aliongeza bao la tatu ambapo hadi mapumiko Yanga walikuwa mbele kwa mabao hayo matatu.


Kipindi cha pili Ndanda walizinduka na kujikakamua na kufanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ngome ya Yanga ilikuwa imara zaidi, Yanga nayo ilijibu mashambulizi hayo kila wakati, ambapo Yanga walisubiri hadi dakika ya 88, ambapo walipata bao likifungwa na kiungo Vicent Bossou akifunga kwa kichwa,ushindi huo sasa unawaweka nafasi nzuri Yanga kwa kufikisha pointi 40 pointi moja mbele ya wapinzani wao Simba wenye pointi 41,


Vinara wa Ligi hiyo Simba wao wanajitupa Uwanjani kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, kumenyana na Ruvu Shooting.

 


Breaking News:MAKOCHA WA AZAM FC WATIMULIWA KAZI,BAADA YA KUSHINDWA KUIPA MAFANIKIO TIMU HIYO..

Azam FC imeawasimamisha kazi makocha wake, Zeben Hernandez pamoja na wasaidizi wake

Zeben na wenzake , wametimuliwa hii leo kufuatia Azam FC kuwa na  mwendo wa kusuasua katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayoongozwa na Simba wenye pointi 41 wakifutiwa na mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 40
Azam FC hadi sasa ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 kibindini huku ikiwa imeshacheza mechi 17.
Katika mechi hizo timu hiyo ya Azam FC imefanikiwa kushinda mechi saba,na kupteza michezo nne pamoja na  sare sita.

MWANASOKA NGULI WA KENYA ALAZWA HOSPITALINI , NDUGU WAELEZA KUENDELEA NAFUU


Mwanasoka maarufu nchini Kenya, Joe Kadenge, amelazwa katika hospitali moja mjini Nairobi baada ya kuugua. 

Nyota huyo mstaafu aliyeiwakilisha klabu ya Afc Leopards na timu ya taifa ya Kenya, alikimbizwa hospitalini mapema wiki hii baada ya kuugua kisukari. 

Wachezaji wenzake wa zamani, George Sunguti na Reginald Asibwa walimsaidia kumfikisha hospitalini baada ya kuzidiwa na maumivu. 

Hata hivyo familia yake inasema kuwa Kadenge amepata nafuu na hali yake inaendelea kuimarika.
Ni mara ya pili shujaa huyo kuugua na kukimbizwa hospitalini . 

Mwezi Oktoba, Kadenge alikimbizwa hadi hospitali ya Meridian mjini Nairobi alipokuwa akitazama mechi ya ligi ya soka ya taifa hilo. 

"Amepata nafuu kwa sasa na mke wake amejiunga naye hospitalini kumsaidia," Sunguti ameliambia gazeti la Nation nchini Kenya.

Wapenzi wa soka nchini humo wamekuwa wakimtakia mzee huyo nafuu. 

Mnamo mwezi Septemba Kenya ilimpoteza kocha na mchezaji maarufu James Sianga aliyefariki baada ya kuugua kwa kipindi kirefu magharibi mwa Kenya. 

ZIARA YA MAJALIWA RUANGWA YAENDELEA ...

 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namilema wialyani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na vikongwe  wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo  akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa , Desemba 28, 2016. (Pichana ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RYAN GIGGS KUCHUKUA MIKOBA YA KOCHA BOB BRADLEY


Kiungo wa zamani wa Manchester United anatarajiwa kumrithi mkufunzi aaliyekuwa mkufunzi wa Swansea Bob Bradley, aliyetimuliwa usiku wa kuamkia leo na Klabu ya Swansea.

Awali, Giggs, mwenye umri wa miaka 43, alihojiwa mara mbili na timu hiyo kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Bradley mwezi Oktoba.


Bradley aliachishwa kazi baada ya kuiongoza Swansea kwa siku 85 pekee na kuiacha katika nafasi ya 19 kwenye ligi.


Ingawa hana uzoefu mwingi, baada ya kustaafu, Giggs aliitumikia Manchester United chini ya David Moyes na kuwa naibu wa kocha, chini ya meneja wa zamani Louis van Gaal.

Nahodha huyo wa zamani wa Wales anadaiwa kufanya mazungumzo na wasimamizi wa Swansea, na mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkins anadaiwa kuvutiwa na Giggs.

Naibu kocha wa Zamani wa United Rene Meulensteen, anaamini Giggs anatosha kuiongoza Swansea.

"Siamini kuwa Giggs hana uzoefu, alipata ujuzi akiwa naibu mkufunzi chini ya Manchester United." Rene Aliiambia BBC Radio 5 Live.

Wengine wanaosakwa na klabu hiyo ni meneja wa Wales, Chris Coleman, mkufunzi wa zamani wa Leicester City Nigel Pearson na aliyekuwa mkufunzi wa Birmingham City manager Gary Rowett.

Hata hivyo, Mrithi wa Bradley anatarajiwa kuchukua usukani baada ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Bournemouth mwisho wa mwezi.
 

Kwa sasa, timu hiyo inayoongozwa na wakufunzi wa muda Alan Curtis na Paul Williams watainoa timu hiyo hadi uteuzi utakapofanywa.

Swansea ilipoteza mechi yake ya saba kati ya mechi 11 kwa kupata kichapo cha 4-1 dhidi ya West Ham ikiongozwa na Bradley
Timu hiyo ina alama 12 baada ya kukusanya pointi 8 pekee na kufungwa mabao 29.

Tuesday 27 December 2016

ASAKARI JESHI NA WANAHABARI WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU KATIKA KILELE CHA UHURU ,MLIMA KILIMANJARO.

Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut.
Safari ilikuwa ni usiku kucha 
Jua likachomoka wakati safari ikiendelea.
Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak.
Matumaini yakaana kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana.
Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji.
Gilmans Point hatiaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.
Miongoni mwa waliofika Gilmans Point ni Naibuu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Ulinzi ,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba.
Safari ya kueelkea Uhuru Peak ikaendelea.
Hatimaye wapandaji wakapita kituo chha Pili ambachi ni Stella na mongoni mwa waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga.
a Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak ,safu ya vilima vikiwa vyenye barafu ndio vilitawala eneo hilo.
Hatimaye safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi ya kupanda Mlim Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika ikafika tamati.

MAREHEMU MPOKI BUKUKU AZIKWA NYUMBANI KWAO MSALATO MKOANI DODOMA

01
Alice Mama wa Marehemu Mpoki Bukuku akisaidiwa kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye Mpoki Bukuku wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma Marehemu Mpoki alifariki hivi karibuni jijini Dar es salaam kwa kugongwa na gari maeneo ya Mwenge.
1
Watoto wa Marehemu Mpoki Bukuku Junior akiongozana na wadogo zake wakiweka shada la maua katika kaburi la baba yao wakati wa mazishi yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma.
2
Junior akiwa ameshikili msalaba kwa majonzi wakati wa mazishi ya baba yake.
3
Mke wa Marehemu Mpoki Bukuku Bi. Lilian na watoto wake wakiaga mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
4
jeneza lenye Mwili wa marehemu Mpoki Bukuku likiteremshwa kaburini.
5
Mbunge wa Singida Mashariki Mh Lazaro Nyalandu akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Mpoki Bukuku.
6
Mke wa Marehemu Bi Lilian akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu mumewe.
7 8
Viongozi wa Dini wakiwa katika ibada hiyo ya mazishi.
9
Ndugu na jamaa waombolezaji wakiomboleza kwa uchungu mkubwa.
10 12
Naibu Waziri Anthony Mavunde pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Mh. Razalo Nyalandu wakiombea mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
13
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
16
Junior akiaga mwili wa baba yake Marehemu Mpoki Bukuku.
17 18
Mama wa Marehemu Mama Alice akiaga mwili wa mtoto wake mpendwa marehemu Mpoki Bukuku.
19
Waombolezaji wakiwa katika mstari wa kuaga mwili wa marehemu.
20
Naibu Waziri Anthony Mavunde pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Mh. Razalo Nyalandu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
21
Naibu Waziri Anthony Mavunde akitoa salam za pole kwa wafiwa.
22
Naibu Waziri Anthony Mavunde akisaini kitabu cha maombolezo.
23
Mpiga picha wa magazeti ya Serikali TSN Habari Leo na Dairly News Bw. Mroki Mroki akitoa salamu za pole kwa wafiwa kwa niaba ya chama cha wapigapicha.
24
Bw. John Bukuku akitoa salamu za pole kwa wafiwa kwa niaba ya Wanamitandao
25
Mwenyekiti wa Press Club ya waandishi wa habari mkoani Dodoma Bw. Chidawali akitoa salamu zake kwa niaba ya wanahabari mkoani humo.
26
Mbunge wa Singida mjini Mh. Lazaro Nyalandu akitoa salam za pole kwa wafiwa.
27
Waombolezaji wakiwa katika mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube