BREAKING

Tuesday, 31 May 2016

LUHWAVI AKAGUA JENGO LA MIKUTANO LA CCM DODOMA LEO

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi (wapili kushoto) akikagua jengo la Mikutano la CCM, Dodoma Convetion Centre leo ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai mwaka huu katika ukumbi huo. Kushoto ni  Ofisa Miliki wa Jengo hilo Tegemeo Saambili 
Luhwavi akitazama hali ya maua kwenye bustani za jengo la ukumbi huo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Tegemeo Saambili (kushoto), alipokagua jengo hilo leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akihoji kuhusu hali ya bustani zinazozunguka jengo hilo
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi hali ya maua kwenye bustani za jengo hilo, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Luhwavi akielekeza namna ya kuboreshwa bustani zinazozunguka jengo la ukumbi huo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizunguka jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Cetre, alipokagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu
Luhwavi akiingia ndai ya ukumbi wa jengo hilo kuona hali halisi
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison (kushoto), akimpa maelezo kuhusu hali ya ndani ya jengo hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipolikagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.
Kaimu Meneja Miliki wa Jengo la Mikutano la CCM la Dodoma Convetion Centre, Christopher Ngalison (kushoto), akionyesha baadhi ya viti ambayo hutumiwa na wajumbe, katika ukumbi huo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (hayupo katika picha), alipolikagua leo Mei 31, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCm, unaotarajiwa kufanyika Juni au Julai Mwaka huu.  Mkuu wa Idara ya Usalama na Maadili Makao Makuu ya CCM, Masudi Mbengula
Bendera ya Taifa na bendera ya CCM zikipepea kwenye jengo hilo la Mikutano la CCM, kama ilivyo kawaida.

Sunday, 29 May 2016

MABINGWA MADRID WATUA NYUMBANI NA KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA



Mabingwa wa Uefa Champions League kwa mara ya 11, Real Madrid wamerejea kwao Hispania na kupokelewa kwa shangwe ile kinoma.

Madrid wamerejea katika jiji la Madrid saa chache baada ya kubeba ubingwa huo kwa mikwaju 5-3 ya penalti dhidi ya wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid.

Mechi ya fainali ilichezwa katika jiji la Milan, kwenye Uwanja maarufu wa San Siro na mechi hiyo kutazamwa na zaidi ya watu milioni 200 duniani kote.






















29 May 2016
Next
This is the most recent post.
Previous

Thursday, 26 May 2016

TAKUKURU KUWAFIKIA WANANCHI WOTE ELIMU DHIDI YA RUSHWA KUPITIA "LONGA NASI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania imebainisha kuwa, itaendelea kutoa elimu kwa kila mwananchi popote pale alipo atafikiwa ilikunufaika katika mapambano dhidi ya rushwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mapema leo Mei 26, Kaimu Mkuu wa sehemu ya Uratibu na utoaji Habari Idara ya Elimu kwa Umma, Makao Makuu TAKUKURU, Bwana. Matai Kilumbi amesema kuwa baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya ‘LONGA NASI’, alisema kuwa, ni kutoa wigo wa kutoa elimu sahihi ya mapambano hayo ya rushwa na pia kupitia kampeni hiyo, watawafikia watu wote kupitia gari maalum la ‘LONGA NASI’ kwani kutakuwa na faida kubwa.
“Mbali na kuzindua huduma hii ya LONGA NASI, pia tumezindua huduma mpya ya 113 ambayo watu watapiga simu ama kutuma ujumbe mfupi ambao utasaidia kushugulikia matatizo ya vitendo vya rushwa” alisema Bw. Matai Kilumbi.
Aidha, aliongeza kuwa, watu wanaweza kutumia huduma hiyo kwa wakati wowote na watahudumiwa moja kwa moja.

DSC_4248Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI' Likiwa mitaani wakati wa huduma hiyo ya LONGA NASI kwa kutoa taarifa ya rushwa -simu ya bure ya 113.
DSC_4244Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI'.
DSC_4251Moja ya gari ambalo linatumiwa na TAKUKURU kufikisha ujumbe huo wa 'LONGA NASI'.
Hivyo, kwa kuendesha kampeni ya ‘LONGA NASI’, Mkakati wa Mawasiliano wa TAKUKURU utakuwa umetekelezwa ipasavyo lakini la muhimu ni kwamba jukumu la kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha umma katika kuzuia na kupambana na rushwa litakuwa limetekelezwa.
HUDUMA MPYA YA KURAHISISHA MAWASILIANO NA TAKUKURU
Sambamba na uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI, TAKUKURU tulizindua huduma mpya itakayowasaidia wananchi kutufikia kwa urahisi kupitia namba za dharura “113” au *113# ambazo ni BURE kama ifuatavyo:
  • Ilivyokuwa kabla ni kwamba mwananchi anaweza kupiga namba “113” kupitia simu yake ya kiganjani au mezani na kuongea na Afisa wa TAKUKURU moja kwa moja kumweleza shida yake au kuripoti tukio la rushwa. Utaratibu au huduma hii ni kupitia mitandao ya TTCL, AIRTEL, TIGO, HALOTEL, VODACOM na ZANTEL;
  • Sasa mwananchi anaweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi yaani “sms” kwenda nambari “113” ili kutoa maoni yake, kuuliza swali au kutoa taarifa.
  • Na pia mwananchi kupitia simu yake ya kiganjani anaweza kutoa taarifa ya rushwa kwa kupiga *113# (USSD) na kufuata maelekezo yatakayofuatia;
OFISI MAALUM YA MAWASILIANO YA DHARURA (PCCB CALL CENTRE)
  • Kutokana na kuanzishwa kwa huduma hizo tajwa, tunaamini kutakuwa na mwitikio mkubwa kwa wananchi kuwasiliana nasi. Hivyo ili kuhakikisha kuwa TAKUKURU tunatoa kutoa huduma hii kwa haraka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ameanzisha ofisi maalum ya MAWASILIANO YA DHARURA (PCCB CALL CENTRE) iliyopo Makao Makuu ambayo itafanya kazi masaa ishirini na manne (24).
  • Lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa za wananchi tunazopewa zinashughulikiwa haraka ikiwa ni pamoja na kuanzisha Uchunguzi.
  • Natumia fursa hii kuwahimiza wananchi kuLONGA NASI bila woga lakini si kwa lengo la kumwonea mtu. Tupatieni taarifa sahihi nasi tutakulinda na tutawashughulikia wanaohusika na tuhuma hizo kwa weleni na haki.
Katika huduma ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia mfumo wa USSD - *113# - Mtoa taarifa ana haki ya kutaka atambuliwe au asitambuliwe na TAKUKURU. Iwapo mwananchi hatapenda kutambulika na TAKUKURU basi ahakikishe kuwa taarifa aliyoiwasilisha itakuwa imejitosheleza kwa kiwango Fulani vinginevyo itatuwia vigumu kupata ushirikiano wa mtoa taarifa katika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma husika.
DSC_4229Kaimu Mkuu wa sehemu ya Uratibu na utoaji Habari Idara ya Elimu kwa Umma, Makao Makuu TAKUKURU, Bwana. Matai Kilumbi akielezea namna walivyojipanga kusambaza elimu dhidi ya mapambano ya rushwa hapa nchini kupitia Huduma za 113 na LONGA NASI. kushoto kwake ni Afisa mahusiano wa TAKUKU, Bi. Angela Mulanduzi. Wakati wa mkutano huo leo Mei 26.2016, Jijini Dar es Salaam.

Wednesday, 25 May 2016

YANGA KUANZA NA WAARABU UGENINI, BAADAE KUMALIZA NA TP MAZEMBE




Juni 17/19 
Mo Bejai (Algeria) Vs Yanga (Tanzania)

Juni 28/29 
Yanga (Tanzania) Vs TP Mazambe (DRC)

Julai 15/17
Yanga (Tanzania) Vs Madeama( Ghana)

Julai 26/27
 Madeama (Ghana) Vs Yanga  (Tanzania)

Agosti 12/14 
Yanga  (Tanzania) Vs Mo Bejaia (Algeria)


Agosti 23/24
 TP Mazembe (DRC) Vs Yanga  (Tanzani

Tuesday, 24 May 2016

WAZIRI NAPE AWAKUMBUSHA WANAMICHEZO NCHINI KUZINGATIA SUALA LA NIDHAMU NDANI NA NJE YA UWANJA ILI KUONGEZA UFANISI

   Baadhi ya wanamichezo wa kutoka Vikundi mbalimbali vya Jeshi wakiwa Jukwaani wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye, amezindua mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ,CDF katika

Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, huku akiwakumbusha wanamichezo wanaoshiriki mashindano hayo suala zima la nidhamu michezoni..

Waziri Nape Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa mashindano ambayo pia ni maandalizi ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya Afrika Mashariki nchini Rwanda ambapo amevipongeza vikosi mbalimbali vya timu za majeshi kwa kuliletea sifa taifa mara zote.

Naye Kaimu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ,Meja Generali Simon Mumwi, akizungumzia mashindano hayo amepongeza mwitikio wa wanamichezo pamoja na kumuahidi waziri Nape kuwa timu za Tanzania zitarejea na ushindi katika Mashindano ya Rwanda.

Awali vikundi mbalimbali vya burudani vilifanya maonyesho, mbalimbali ikiwepo ngoma, bendi za muziki , ambapo baadae Waziri Nape alifungua rasmi mashindano hayo kwa mchezo wa soka kati ya timu ya JKT na Tembo 


YANGA USO KWA USO NA TIMU YA ULIMWENGU, TP MAZEMBE MICHUANO YA SHIRIKISHO HATUA YA MAKUNDI AFRIKA


 KIKOSI CHA YANGA


WACHEZAJI WA TP MAZEMBE


Timu ya Yanga  imepangwa kundi la A katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mabingw wa zamani barani,Afrika  TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.

Kundi B linaundwa na timu za Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za Morocco.
 

Ratiba hiyo inamaanisha Yanga itakutana na timu ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC, katika mchezo wa awali.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika kundi A kuna timu za Zesco United ya Zambia, Al Ahly ya Misri, Asec Mimosa ya Ivory Coast, Waydad Casablanca ya Morocco, wakati Kundi B kuna Enyimba ya Nigeria, Zamalek ya Misri, ES Setif ya Algeria na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube