Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akiangalia namna utengenezaji huo unavyoendelea kwa upande wa nje wa majokofu hayo
Mtaalam wa upande wa Mochwari hiyo ya Tumbi akitafakari jambo wakati wa ujio huo wa Naibu Waziri Dk. kigwangalla
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya
Mkoa wa Pwani-Tumbi kuanza kutumia jokofu moja lenye uwezo wa kuchukua
miili nane (8) katika chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) ya
Hospitali hiyo baada ya kuridhishwa na hatua iliyofikiwa baada ya
kutembelea kwa mara ya pili kuikagua, tokea alipoipa masaa 72 ifungwe
na ifanyiwe matengenezo.
Dk.
Kigwangalla alifika hospitaalini hapo majira ya saa nane mchana na
kisha kwenda moja kwa moja kwenye jingo hilo la Mochwari na kukuta
mafundi wakiendelea na matengenezo kwa upande wa majokofu ambayo
yalikuwa hayafanyi kazi na kusababisha matatizo hata Naibu Waziri
kuagizwa kufungwa ma siku tatu ili uongozi huo ufanyie matengenezo.
“Nilitoa
masaa 72, muwe mumefanyia kazi tatizo hili. Na leo hii nimerudi tena
kukagua kuona utekelezaji wa agizo langu kama mumelifanyia kazi. Hivyo
kwa kuwa tayari ili jokofu moja limeanza kutengamaa nalifungulia lianze
kazi mara moja na la pili lianze kazi pia litakapokamilika mutujulishe
haraka sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo kwa
uongozi wa Hospitali hiyo ya Tumbi.
Ziara
hiyo katika kukagua utekelezaji wa Mochwari hiyo ya Tumbi, ameifanya
jana Machi 13.2016 akiambatana na maafisa wa Wizara yake hiyo ambapo pia
alipata kutembelea Hospitali nyingine ya Jijini Dar es Salaam ya
Sanitas ambayo imefungiwa kutoa huduma kwa upande wa chumba cha Upasuaji
kutokana na kutokidhi vigezo.
Hata
hivyo kwa upande wa Hospitali Dk. Kigwangalla alieleza bayana kuwa,
alipata taarifa juu ya uongozi wa Hospitali hiyo kuendelea na huduma za
upasuaji lakini hakukuta hali hiyo na kuendelea kusisitiza huduma hiyo
isifunguliwe mpaka hapo watakapokamilisha vigezo vya Wizara juu ya
Chumba chaa upasuaji kinavyotakiwa kiwe.
No comments:
Post a Comment