Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanawake unaofanyika nchini Marekani ulioanza jana Machi 14-24, wakiwa nje ya jengo la Umoja wa Mataifa unapofanyika mkutano huo
Pichani ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Masuala ya wanawake, wazee na watoto wa Tanzania, Mh. Ummy Mwalimu akiwasilisha mada kuu ambaapo aliwakilisha kundi la Afrika katika mkutano huo mkubwa unaoendelea nchini Marekani.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo wa #CSW60
Bara
la Afrika na hasa wanawake ndio wanaobeba mzigo zaidi wa madhara ya
mabadiliko ya tabianchi, huku wakinyimwa fursa ya kushiriki katika
kutafuta suluhu kwa tatizo hilo, ameeleza leo Ummy Mwalimu, Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Masuala ya wanawake, wazee na watoto wa
Tanzania.
Bi
Mwalimu amesema hayo akihutubia kikao cha 60 cha Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 kwa niaba ya kundi la nchi za
Afrika, akisisitiza umuhimu wa kushirikisha zaidi wanawake katika
uongozi wa kimataifa kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.
"Wanawake
wanapaswa kuweza kuongoza katika ngazi za kitaifa na serikali za mitaa.
Ubunifu wao, ujuzi wa kiasili, matarajio yao yanaweza kusaidia katika
kubuni na kushawishi suluhu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.”
Aidha
amezungumzia suala la kilimo ambacho hushughulisha wanawake zaidi,
akisema la msingi ni kusaidia sekta binafsi ili kukuza ukuaji wa uchumi
katika sekta hiyo na hivyo kuwezesha wanawake.
No comments:
Post a Comment