Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso akiwatambulisha wasanii kwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (kulia) wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi
Msanii wa filamu ya Shoe Shine na Samaki Mchangani, Amri Shivji akitoa shukrani zake kwa Serikali. Shivji naye filamu yake ya Samaki Mchangani iliweza kushiriki katika tuzo hizo za AMVCA 2016, kama filamu ya Kiswahili.Msanii Single Mtambalike 'Rich Rich' akizungumza machache juu ya ushindi wake ambapo pia ameipongeza Serikali kwa ushirikiano waliowapa hadi kufikia hapo.
Msanii wa filamu ambaye naye filamu yake ilishiriki katika tuzo hizo za AMVCA 2016 akitoa shukrani zake kwa Serikali
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati) akizungumza juu ya kuwapongeza wasanii Rich Rich na Lulu Michael kwa ushindi wao katika tuzo za AMVCA 2016 zilizofanyika nchini Nigeria mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa Wizara hiyo.. Mapema leo 7 Machi.2016
Mkutano huo ukiendelea...
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti maalum cha pongezi, Msanii wa filamu Amir ShivjiWaziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akitoa vyeti kwa wasanii waliofanya vizuri.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi Joseph Lukaza Mwakilishi wa Proin akipokea cheti kwa niaba ya msanii Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye bado hajarudi kutoka Nchini Nigeria.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti Msanii Rich Rich kama pongezi kwa Serikali. Kulia anayeshuhudia ni Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi.2016
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akipokea tuzo hiyo kutoka kwa msanii Rich Rich.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa amebeba tuzo hiyo kama ishara ya kuwawakilisha watanzania wote.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye na Msanii Rich Rich (katikati ) wakiwa katika picha ya pamoja wasanii wengine na viongozi wa Wizara hiyo.
Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso akipiga picha ya ukumbusho na Msanii Rich Rich wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi.2016. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Akitoa
pongezi hizo mapema leo 7 Machi.2016, Waziri wa Habari, Mh. Nape
Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na wasanii mbalimbali wa filamu
nchini waliowasindikiza washindi wa tuzo hizo za African Magic Viewers’
Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria,
Akiwemo mshaindi wa tuzo ya filamu Bora ya Lugha ya Asili (Best Local
Language -Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’, Msanii Single
Mtambalike ‘Rich Rich’ pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAFF),Simon Mwakifwamba ambapo Waziri aliwapongeza kwa mshikamano wao
huo waliouonyesha na hata kurudi kutoa pongezi.
Waziri
Nape amebainisha kuwa, awali Rich Rich kabla ya kwenda Nigeria,
alipata Baraka kutoka kwake hivyo hata kurejea kutoa shukrani ni jambo
jema huku akieleza kuwa, Serikali itahakikisha inawalea wasanii katika
umoja pamoja na kuweka mazingira mazuri ya ufanisi katika shughuli zao
ikiwemo kuandaliwa Sera, kanuni na misingi ya sharia katika kuifanya
tasnia ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi na yenye kuleta fursa za ajira
kwa wasanii ndani na nje.
“Kwa
nafasi yangu ya Uwaziri. Nitahakikisha nawapigania wasanii kufikia
malengo tuliyoyakusudia. Hii ni paamoja na kuwa na Sera madhubuti na
kuzuia mianya ya wafujaji wa kazi za Wasanii wa Tanzania. Serikali ya
awamu ya tano kupitia kwa Rais wetu Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza
na ili la stika za TRA
na munashuhudia wenyewe Mamlaka ya Mapato inavyopambana na watu
wanaorudisha maendeleo ya wasanii nyuma kwa kufunga maduka yao huu ni
mwanzo tutapambana mpaka mwisho katika hili” alieleza Mh.Nape na kupaata
pongezi kutoka kwa wasanii wenyewe ambao waliweza kushangilia kwa kauli
hiyo ya matumaini huku wakipiga makofi.
Aidha,
katika tukio hilo, Serikali imeweza kuwatunukia wasanii hao walioshinda
tuzo hizo za AMVCA 2016 vyeti maalum vya shukrani hii ni pamoja na
wasanii wote ambao filamu zao pia zilienda kushindanishwa huko pamoja na
waandaaji waliowezesha filamu hizo kwa mchango wao mkubwa.
Katika
tuzo hizo mbali na Rich Rich, kushinad tuzo hiyo, Msanii mwingine
aliyeshinda ni pamoja na Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo
ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia
filamu yake ya ‘Mapenzi’.
No comments:
Post a Comment