Wafanyakazi wanane wa mamlaka ya bandari kitengo cha makasha ya bidhaa,yaani CONTAINER'S,wamekimbia ajira zao kufuatia serikali kuwakamata wenzao 7 wanaotuhumiwa kuwa vinara wa kuikosesha serikali mapato kwa kuyapitisha kinyemela makasha hayo bila ya kulipiwa ushuru wa forodha.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi bandarini hapo,waziri wa uchukuzi,ujenzi na mawasiliano,Proffessa MAKAME MBARAWA,alisema kuwa wafanyakazi hao walikimbia baada ya tume maalum iliyoundwa ili kufuatilia upotevu wa makasha hapo bandari na kugundua makasha 300 hayaonekani kama yamepitia njia sahihi za kutolewa katika bandari kavu,kugundua kuwa kuna mengine 11,884 yalipotea kwa mtindo uleule wa yale ya awali.
Amesema inaonekana kuwa wafanyakazi hao walikuwa na ushirikiano na mawakala wa makasha wasiokuwa waaminifu kwa kushirikiana kuidanganya mamlaka ya mapato nchini,TRA,ikishirikiana na wafanyakazi wasio waaminifu wa TRA,pamoja na mamlaka ya Bandari kuhusu ulipaji wa WHARFAGE(TOZO YA BANDARI) huku wakijua kuwa ni kosa.
Aidha amesema kuwa mawakala wa forodha 243 wamepewa siku 7 kukamilisha malipo ya makasha na magari yaliyotolewa bandarini hapo bila ya kulipiwa tozo ya bandari kufanya hivyo katika muda huo vinginevyo serikali italazimika kuwakamata na kuwafikisha polisi ili walipe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa kufanya biashara na mamlaka ya bandari.
Kwa upande wake naibu waziri wa wizara hiyo,Injinia EDWIN NGONYANI,amesema kuwa kuna malalamiko kuwa wapo mawakala wa forodha ambao wanadai wamelipia fedha za tozo lakini bado wanahesabiwa kuwa hawajalipa,amewataka kuwasilisha nyaraka stahiki zitakazoonesha kuwa wamelipia tozo hizo kihalali ili hatua stahiki zichukuliwe.
Akihitimisha kuwasomea taarifa hiyo waandishi wa habari,waziri Professa Mbarawa amesema serikali haitamvumilia mfanyakazi yeyote wa mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini awe mkubwa au mdogo ambae ataendelea na kujihusisha na upotevu wa mapato ya mamlaka ya bandari hiyo pia inahusisha mawakala wote wa forodha ambao wataendelea kujihusisha na wafanyakazi wa mamlaka ya bandari kutoa mizigo bila ya kulipa tozo watafutiwa leseni zao.
No comments:
Post a Comment