Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi Mugwe Mbabe ambaye ni
Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara
baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo
wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya
kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama
wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis
Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato
mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke
mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili
nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara
baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
(82) Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara
baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
(82) Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba
huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili
nyumbani kwake Chato mkoani Geita
Mdogo wa Marehemu Deodatus
Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa
pole na kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016
ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole
kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee
maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani
yake.
Rais Magufuli pamoja na kuwapa
pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao pia
amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na
kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana
na mifarakano.
”Unapotokea msiba kama huu
katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama
mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha
mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana
kama enzi za uhai wa mzee”
Aidha Rais Magufuli amemuelezea
Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini hapa na
miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare
zake za shule wakati akisoma.
Kwa upande wake Mdogo wa marehemu
ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni msemaji
wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana
nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha
kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.
Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
29 Desemba, 2016