BREAKING

Thursday 12 November 2015

RC MAHIZA AUTAKA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF) KUTOA ELIMU ZAIDI KWA WANANCHI JUU YA UMUHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

MKUU WA Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani hapa kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)ili kuweza kuongeza wigo mpana wa wanachama ambao wataweza kunufaika na huduma zao.

  Alitoa wito huo jana wakati akipokea mashuka 150 yaliyotolewa na mfuko huo vyenye thamani ya shilingi milioni tatu yaliyotolewa na Mfuko huo kwa ajili ya vituo vitatu vya afya vya Mkinga, Maramba na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga ambavyo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto ya uhaba wa mashuka. 



No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube