Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bwana Rished Bade na kumteua Bwana Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam, jioni hii imesema Rais Magufuli amemtaka Bwana Rished Bade kumpa ushirikiano wote kaimu Kamishna Mpango katika Uchunguzi kuhusu makontena 349 yaliyotoka Bandarini bila taarifa zake kuwepo katika mamlaka ya mapato Tanzania .
No comments:
Post a Comment