BREAKING

Monday, 23 November 2015

SHEREHE ZA MIAKA 54 YA UHURU RAIS AFUTA GWARIDE ASEMA SASA SIKU HIYO ITATUMIKA KUFANYA USAFI

              Rais John Pombe Magufuli

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli, amefuta sherehe za Uhuru za desemba tisa mwaka huu ambazo zilikuwa zikifanyika kila mwaka na badala yake ameagiza siku hiyo itumike kufanya usafi kwa kila mwananchi.

Rais amesema ni aibu kwa taifa kuadhimisha miaka 54 ya uhuru mwaka huu huku likikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa kiasi kikubwa unasababishwa na uchafu, na ameagiza watendaji wote wa halmashauri na manispaa nchini kuahikikisha wanatayarisha vifaa vya kufanyia usafi ili kila mwananchi aweze kushiriki.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema fedha ambazo zingetumika kwenye maadhimsho ya sherehe za Uhuru mwaka huu zitaelekezwa kwenye maeneo ambayo rais ataona zina mahitaji sana.

Wakati huo huo Balozi Ombeni Sefue amewataka watumishi wote wa Umma kuanza kuvaa Beji zenye Majina yao kwenye nguo zao kutoa fursa kwa wananchi kujua nani anamhudumia.


Kuhusiana na safari za nje kwa watumishi wa umma, Balozi sefue ana fafanua

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube