Watu watano wamefariki dunia pamoja na mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, bilionea Vichai Srivaddhanaprabha baada ya helikopta waliyokuwa wamepanda kuteketea kwa moto.
Mmiliki wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, mwenye umri wa miaka 60, ambaye aliinunua klabu hiyo kwa Pauni Milioni 39 mwaka 2010 na kuiwezesha kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England mwaka 2016 atakumbukwa kama mtu wa kipekee na muungwana.
Mlimbwende, Nursara Suknamai, Msaidizi wake, Kaveporn Punpare na rubani, Eric Swaffer, ambaye hapo kabla alisafirisha familia ya kifalme, na mpenzi wake na rubani mwenzake wake, Izabela Roza Lechowicz wote wamefariki kwenye ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment