Baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa jana Uwanja wa Taifa, umeonekana kuwachanganya viongozi wa Simba kwa furaha, Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amehoji ni nani mwingine anayekuja ili aweze kushushiwa mvua ya mabao.
Manara alisema kuwa kwa mwendo huu wa Simba kuna timu itapigwa mabao mengi zaidi ya hayo matano kutokana na aina ya wachezaji waliopo Simba, mbinu za Kocha, Patrick Auusems kueleweka.
"Simba ni klabu kubwa lazima uiheshimu, nilikwambia ntakujibu baada ya dk 90, umepapapaswa halafu square unashtka, hii ndio Simba tunang'ata, nani mwingine anakuja ? kwa mwendo huu kuna mtu atapigwa nyingi sana zaidi ya bao 5," alisema.
Simba imefanikiwa kuendeleza rekodi yake ya kufunga mabao mengi kwenye ligi ndani ya mechi moja, kwani kwa mechi zote tano ambazo zilichezwa jana timu nyingi zilishinda kwa idadi ya bao 1 huku Simba ikishinda kwa mabao 5-0..
No comments:
Post a Comment