Habari njema kwa kuwa Watanzania wataishuhudia timu ya taifa, Taifa Stars Mubasharaa ikiivaa Cape Verde ugenini, kesho.
Mechi hiyo ya kuwania kufuzu Afcon, itaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya SuperSport10 kupitia king'amuzi cha Dstv.
Katika taarifa iliyotolewa na Multichoice Tanzania, mechi hiyo itarushwa moja kwa moja kutoka mjini Praia kuanzia saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Watanzania wengi wapenda michezo na hasa soka walikuwa wakiuliza kama mechi hiyo itarushwa moja kwa moja lakini sasa wana uhakika wa mambo kwamba wataishuhudia mechi hiyo muhimu ya kuwania kufuzu kucheza Afcon, mwakani.
No comments:
Post a Comment